Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 11, 2014

Spika Makinda amuaga Mwakilishi Mkazi wa UNDP, amkaribisha Balozi wa Cuba



Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda Mb akiwa na mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania anayemaliza muda wake Bwana Abeeric Kacou (kushoto) mara baada ya Mwakilishi Mkazi huyo kufika Ofisini kwa Spika leo kwa nia ya kumuaga.
“Kwaheri na asante kwa kazi nzuri na karibu tena Tanzania ”…. Ndivyo Spika anavyomwambia Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bwana Kacou baada ya kumaliza miaka minne ya utumishi hapa nchini Tanzania.
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda, Mb, akimkaribisha Balozi mpya wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo (kushoto) ofisi kwake leo ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kuendeleza ushirikiano wanchi mbili hizi. Picha na Owen Mwandumbya - Bunge.

No comments:

Post a Comment