Gazeti la Tanzania Daima la tarehe 23 Januari, 2013 liliandika makala inayosomeka "JK AMNUSURU MFUNGWA WA EPA". Gazeti hilo lilidai mfungwa wa
kesi ya EPA Ajay Somani ametolewa gerezani kwa njia ya kutatanisha
wakati wafungwa wengine waliokuwa kesi moja wanaendelea kusota gerezani.
Maelezo
mafupi kuhusu suala hilo ni kwamba mfungwa Na. 74/2012 Ajay Suryakant
Somani tarehe 22 Novemba, 2012 alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu shauri la Jinai Na. 1164/2008 kwa kosa la "Obtaining Money by False Pretence c/s 302 of the Penal Code".
Watuhumiwa
wenzake katika kesi hiyo walikuwa Sophia Joseph Lalika, Ester Komu na
Emmanuel Mwakyosa. Hawa walikuwa wanakabiliwa na shtaka la "Occasioning Loss to a Specified Authority". Hawa walihukumiwa
kifungo cha miaka mitatu au faini shilling! milioni tano (Tzs.5,000,000/=) kila mmoja. Wafungwa
wawili Ester Komu na Emmanuel Mwakyosa walilipa faini siku hiyo hiyo
mahakamani na kuachiliwa huru. Mfungwa Sophia Joseph Lalika kwa kuwa hakulipa
faini
hiyo mahakamani alipelekwa gerezani na tarehe 23/11/2012 alilipa
faini hiyo na kuachiliwa huru. Hivyo madai yaliyotolewa kwamba bado wanasota gerezani siyo ya kweli.
Kuhusu
Mfungwa Na. 74/2012 Ajay Suryakant Somani wakati akiendelea na kifungo
chake gerezani alipata mapunguzo ya 1/6 ya kifungo chake kwa msamaha
wa Rais uliotolewa kwa wafungwa tarehe 9 Desemba, 2013 wakati wa kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa nchi yetu. Mapunguzo haya ya 1/6 ni zaidi ya mapunguzo ya kawaida 1/3 yanayotolewa chini ya Sheria ya Magereza ya mwaka 1967. Kutokana na msamaha huo kifungo chake kupunguzwa kwa nusu (1/3 + 1/6 = 1/2) yaani mwaka mmoja na kwa hali hiyo kustahili kuachiliwa huru tarehe 9/12/2013.
Wafungwa wengine waliotajwa No.247/2011 Farijala Shabani anayetumikia kifungo cha miaka kumi na moja (11) na Na. 345/2011 Rajabu Maranda anayetumikia
kifungo cha miaka kumi (10) nao walinufaika na msamaha huo wa Mhe. Rais
lakini waliendelea kubaki gerezani kutokana na urefu wa vifungo vyao.
Hivyo Gazeti husika lifute kauli hiyo kwa kuwa waliachiliwa huru kwa
mujibu wa sheria na kwa sasa ni raia huru.
John C. Minja
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
23 Januari, 2014
No comments:
Post a Comment