AHMED Z. MSANGI - SACP |
TAARIFA YA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE”
TAREHE 08.01. 2014.
WILAYA YA CHUNYA
- WIZI WA GARI.
MNAMO TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO ENEO LA KUEGESHA
MAGARI YA KAMPUNI YA SUNSHINE
MINING LTD KATIKA KIJIJI CHA MATUNDASI,
KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA
KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA
MKOA WA MBEYA. MSABAHA
S/O RASHID KAFULAMA, FUNDI MKUU WA
KUTENGENEZA MAGARI WA KAMPUNI HIYO
ALIIBA GARI T.421 CHG AINA YA
TOYOTA
L/CRUISER SINGLE CABIN RANGI NYEUPE CHASES NO JCLB-715407036705 LENYE THAMANI
YA USD 35,000 NA KWENDA MAHALI
KUSIKOJULIKANA. MBINU NI KUJARIBU
KUENDESHA GARI HILO BAADA YA KULIFANYIA
MATENGENEZO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA
MAHALI ALIPO MTUHUMIWA PAMOJA NA GARI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
WILAYA
YA MBARALI - AJALI YA
MOTO.
MNAMO TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 20:15HRS HUKO KATIKA SHULE YA
WASICHANA YA SEKONDARI IGUMBILO
INAYOMILIKIWA NA KANISA LA LUTHERANI, ILIYOPO
KATA YA CHIMALA, TARAFA YA ILONGO WILAYA YA MBARALI
MKOA WA MBEYA. BWENI MOJA LA SHULE HIYO LILIUNGUA MOTO NA KUTEKETEZA MALI ZOTE ZILIZOKUWA NDANI YA BWENI HILO. CHANZO BADO KUFAHAMIKA, INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA NI
HITILAFU YA UMEME. HAKUNA MADHARA
YA KIBINADAMU YALIYOTOKEA. THAMANI
HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO
KUFAHAMIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA KUCHUKUA
TAHADHARI DHIDI YA MAJANGA YA MOTO.
WILAYA
YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA
MOSHI
[GONGO].
[GONGO].
MNAMO TAREHE 07.01.2014 MAJIRA YA SAA
12:50HRS HUKO KATIKA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI CHA MPONZI KILICHOPO KATA YA KAGERA, TARAFA YA SISIMBA
JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA /MSAKO WALIMKAMATA
PRISCA D/O GODWIN, MIAKA 27, KYUSA,
MKULIMA, MKAZI WA MTAA WA KAGERA AKIWA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO
WA LITA 1.5. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI
NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA
POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
Signed
by:
[AHMED Z. MSANGI - SACP].
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment