Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent
Kone akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango wa Tiba kwa kadi (TIKA)
katika halmshauri ya manispaa ya Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Aque Vitae Resort mjini Singida. Kushoto ni mkuu wa wilaya
ya Singida, Queen Mlozi.
Meneja msaidizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya mkoa wa Singida, Isaya Shekifu, akizungumza muda mfupi kabla ya
kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Singida.Dk.Parseko Kone, kuzindua mfuko wa
Tiba kwa kadi (TIKA) katika manispaa ya Singida. Walioketi kutoka kulia
ni mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda na Mstahiki Meya wa manispaa
ya Singida,Sheikh Salumu Mahami.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa
Singida,Yahaya Nawanda, akitoa mada yake iliyohusu mfuko wa afya ya
jamii (CHF) kwenye mkutano wa wadau wa afya wa manispaa ya Singida.
Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,(wa
kwanza kulia) akisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano wa
wadau wa afya wa manispaa ya Singida. Wa kwanza kushoto,ni mstahiki meya
wa manispaa ya Singida,Sheikh Mahami.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na madiwani wa manispaa ya Singida.Walioketi wa kwanza kulia ni Diwani wa viti maalum Yagi Kiaratu na anayefuatia ni mstahiki Meya wa manispaa ya Singida,Sheikh Salum Mahami.Kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda na mkuu wa wilaya ya Iramba na Queen Mlozi, mkuu wa wilaya ya Singida.(Picha na Nathaniel Limu). |
Na Nathaniel Limu, Singida
WADAU wa afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa kauli moja
wameridhia kuanzishwa kwa Mpango wa Tiba kwa Kadi (TIKA) katika Manispaa
hiyo.
Wadau hao wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa mpango wa TIKA una
manufaa mengi ikiwemo mwananchi baada ya kulipa ada ya uanachama,
atakuwa na haki ya kupata huduma za matibabu ndani ya Manispaa kwa mwaka
mzima.
Kwa mujibu wa Meneja Msaidizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
Mkoani Singida, Isaya Shekifu mpango wa TIKA ambao unafafana na Mfuko wa
Afya ya Jamii (CHF) unatumika mijini tu.
Shekifu amesema uanachama wa TIKA ni wa mtu mmoja mmoja, wakati ule wa CHF, ni wa familia au kikundi.
“Kwa sasa hapa Manispaa ya Singida, baada ya mpango huo kupata baraka
ya kuanzishwa tunaendelea na mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya CHF
kwenda kwenye Tiba kwa Kadi (TIKA)”,alifafanua Shekifu.
Meneja Msaidizi huyo amesema baada ya kukamilika kwa sheria ndogo
itakayotawala uendeshaji wa TIKA, mpango huo utaanza rasmi mapema
iwezekanavyo mwaka huu.
Akizindua mpango huo wa Tiba kwa Kadi (TIKA) katika Manispaa ya Singida
juzi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone amesema mpango wa TIKA
utawahakikisha wakazi wa Manispaa ya Singida na viunga vyake mwanzo
mpya wa kupata huduma za matibabu zenye uhakika.
Hata hivyo, Dk. Kone aliagiza viwango vya uchangiaji vya TIKA
zitazingatia uwezo wa mwananchi kulipia pia vitazingatia hali ya sasa ya
huduma za matibabu.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa kuwa suala la TIKA
ni la hiari wananchi watajiunga kwa wingi endapo watahamasishwa
kikamilifu.
“Kila mmoja hapa awe balozi mzuri kwa kuhamasisha wannachi wajiunge na
mpango huu mara baada ya sheria ndogo kupitishwa. Manispaa ihakikishe
huduma zinakuwa bora katika vituo vyote ikiwa ni pamoja na lugha nzuri
kwa wananchama”,amesema Dk.Kone.
No comments:
Post a Comment