Mkuu wa
mkoa Iringa Dr Christine Ishengoma akiongea na waandishi wa habari
katika ukumbi wa mikutano ofisini kwake tar,10/01/2014 wakati akitoa
taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha miezi sita
Julai-Desemba 2013.
Pichani
waandishi wa habari mkoa wa Iringa na maafisa ofisi ya Mkoa
wakimsikiliza Mkuu wa Mkuu Dr Christine .G.Ishengoma wakati akito
taarifa ya kazi.
Afisa
kilimo Mkoa wa Iringa Paulo Msangi akifafanua jambo kuhusu Idara yake
wakati wa maswali na majibu baada ya taarifa ya mkuu wa mkoa Iringa.
Taarifa hiyo ilio jumuisha shughuli zifanyikazo katika mkoa wa Iringa kwa ujumla kama Sekta ya kilimo na uzalishajimali.
kwamapinduzi ya kilimo kumekuwa na ongezeko la matumizi ya zana za
kilimo Matrekta makubwa,madogo na zana zakukokotwa na wanyama kazi kwa
asilimia 0.23 kwa mwaka 2013-2014.
kulikopelekea ongezeko la uzalishaji mazao kwamfano mahindi kutoka tani 549,363.5 mpaka 676,936.
Hivyo kumeongeza uzalishaji mazao yote kwajumla kwakuwa kulikuwepo na upatikanaji wa pembejeo na matumizi yake kwa wakulima.
kwa upande wa
umwagiliaji jumla ya hekta 2,080 za mpunga zinalimwa katika skimu za
umwagiliaji nakufanya kuwe na ongezeko la asilimia 46% taka 31% kuliko
pelekea kuvuna tani 58,370.
Mapinduzi ya mifugo na mafunzo kwa wafugaji elimu imetolewa katika
vijiji 34 vya mkoa wa Iringa nyanda za malisho na Afya ya mifugo pamoja
na Mradi wa kopa Ng'ombe lipa Ng'ombe. na vikundi 47 vilipata Elimu.
Pamoja na hayo taarifa hiyo imejumuisha Sekta
za Utalii,Viwanda,Biashara na masoko pamoja na kuendelea kuhamasisha
Jamii kutumia bidhaa zinazo zalishwa ndani na kuwajengea uwezo wa
ujasiliamali.
Sekta ya miundo mbinu kumekuwepo na upimaji wa mipaka ya vijiji,Mashamba,Viwanja na utoaji wa Hati miliki
Kuandaa michoro 8 ya Mipangomiji na kupima viwanja2160 katika halmashauri Wilaya za Iringa Manispaa na Mufindi.
Matengenezo ya barabara maeneo korofi jumla ya km.218.7 katika
Halmashauri za Iringa ,manispaa na kilolo zinahitaji matengenezo ya
kawaida zipo katika hatua ya kuwapata wakandarasi na Km.22 katika wilaya
ya Mufindi zimetengenezwa.
Pia kuna matengenezo maalumu jumla ya km.83.16 katika halmashauri
zote zinafanyiwa matengezo ya muda maalumu na zipo katika hatua
mbalimbali za Ujenzi.
Sekta ya uwezeshaji wananchi kiuchumi jumla ya saccos 2 zimeundwa na
kufanya jumla ya saccos 270 pia mikopo yenye thamani ya Tsh.11,525,000/=
kwenye halmashauri ya Wilaya ya Iringa
Uboreshaji wa elimu ya msingi na Sekondari, Afya na huduma ya maji,
pia kuwaongezea uwezo wananchi kukabiliana na majanga wananchi
wanaendelea kupewa elimu katika halmashauri zote.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment