Marehemu Zainab Buzohera |
Siku ya Ijumaa Jan 3, 2014 baada ya kuanza kujisikia vibaya Marehemu
Zainab alikwenda Hospitali ya Doctor's Community iliyopo Lanham,
Maryland ambayo ni kama maili 7 kutokea nyumba kwake kwenye mji wa
Bladensburg, Maryland aliokuwa akiishi enzi ya uhai wake. Siku hiyo saa 5
usiku marehemu alifika hospitali kitengo cha Emergency baada ya kuanza
kujisikia kushindwa kupumua na baada ya kuchekiwa na madaktari walimkuta
na tatizo la homa ya mapafu (Pneumonia stage 3).
Baada ya madaktari kugundua tatizo la Zainab ni kubwa, Siku ya Jumamosi
Jan 4, 2014 Mpendwa wetu alipatiwa kitanda kwenye wodi ya wagonjwa
mahututi (ICU) huku akiwekewa mashine ya Oxygen ili kumsaidia kupumua.
Mpendwa wetu alishawahi kulazwa hospitali siku za nyuma lakini
kinachowashangaza wengi hasa marafiki zake wa karibu ni jinsi
alivyowapigia simu karibu kila mmoja na kuwaeleza kulazwa kwake siku
hiyo jambo lililotafsiliwa na wengi wakiwemo marafiki zake kwamba
alishajua mauti itamkuta na kuwapigia simu huko ilikuwa anawaaga.
Mmoja wa marafiki zake anayeishi Maryland alielezea siku ya harambe
kwamba Zainab ameishaugua kabla ya hapo laikini hajawahi kumpigia simu,
hii ilikua ni mara ya kwanza na alipokwenda hospitali anakumbuka maneno
aliyoambiwa na marehemu kwamba " hewa hiyo itumie wakati unanafasi
angalia mimi pamoja na hewa yote hiyo kuwepo nimewekewa Oygen"
Baadae madaktari walimkataza asiongee na simu kwani anahitaji kupumzika
badala yake Zainab alianza kuwatext marafiki zake kuwaelezea jinsi
anavyoendelea. Japokuwa baadae kutexti nako alikatazwa na text ya mwisho
alimtextia Dullah akimwambia amekatazwa asitext tena. Ndipo ilipofika
saa 2 usiku siku hiyo ya Jumamosi Jan 4, 2014 mpendwa wetu aliaga Dunia.
Dullah na Zainab walikuwa pamoja si chini ya miaka 17, tangia Ukonga
Banana walipokuwa wakiishi jirani na Saidi Mwamende na dada yake Nuru na
mpendwa wetu Zainab ambaye ndiye aliyetangulia kwenda Marekani mwaka
2000 na mwaka uliofuatia Dullah akaungana naye.
Mpendwa wetu Zainab na Dullah walishaoana kiserikali na walikuwa na
mipango ya kwenda wote nyumbani kati ya mwezi March au April kwaajili
yakutia ubani ndoa yao.
Zainab sisi tulikupenda lakini Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema amekupenda zaidi, daima utakumbukwa, mama, baba, kaka, dada, wadogo zako, ndugu, jamaa na marafiki bila kumsahau kipenzi chako cha rohoni Dullah.
Zainab sisi tulikupenda lakini Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema amekupenda zaidi, daima utakumbukwa, mama, baba, kaka, dada, wadogo zako, ndugu, jamaa na marafiki bila kumsahau kipenzi chako cha rohoni Dullah.
Dullah na Zainab Enzi hizo za Ukonga Banana |
Mwili wa mpendwa wetu uliondoka siku ya Alhamisi Jan 9, 2014 badala ya
Jumatano na unatarajiwa kufika Dar es Salaam, Tanzania siku ya Jumamosi
Jan 11, 2014 na maziko yatakuwa Jumapili siku inayofuata. Wasindikizaji
wao waishafika tangia Alhamisi.
Inna lillahi wainna ilayhi rajiuun
Inna lillahi wainna ilayhi rajiuun
No comments:
Post a Comment