WANANCHI
wenye hasira wa Kijiji cha Kisiwa Kata ya Kiloka Wilaya ya Morogoro
Vijini jana usiku wamewauwa kisha kuwachoma moto watu watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi.
Akizungumza
na Mtandao huu shuhuda wa tukio hilo Bw Shabani Mango alisema majambazi
hao walivunja nyumba ya mkazi mmoja wa kijijini hicho na kuiba shilingi
490,000.
"Jamaa walifka hapa majira ya saa 8 usiku wakiwa na pikipiki Feko yenye namba za usajiri
T310 BTC
wakipakizana mshikaki,walivunga geni na kuingia ndani ambapo walipora
kiasi hicho cha fedha"alisema Mango na kuongeza" Fedha hizo Mwalimu Said
Swale Tajiri alizikopa jana mchana kwenye saccos ya Moboto kwa lengo la
kumlipia ada mdogo wake anayesoma jijini Dar es salaam leo ijumaa
alipanga kwenda Dar kulipa ada nahisi jamaa walipata taarifa kwamba
Ticha ana mzigo ndani"alisema Bw Mango.
Akihojiwa
na mtndao huu afisa mmoja wa jeshi la polisi alithibitissha kutokea kwa
tukio hilo na kuwataja majambazi hao kuwa ni Emmanuel Mlapoli na Kessy
Benno ambaye ni boda boda naye pack Pangawe jeshini.
''Jambazi
mmoja jina lake bado halijafahamika na kwamba eneo la tukio tulikuta
pikipiki aina ya Feko yenye namba za usajiri T 3710 BTC mali ya marehemu
Kessy Benno ambaye ni makzi wa Kingulwila stesheni manispaa ya
Morogoro'alisema Afande huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwakuwa sio
msemaji wa jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment