Mwanamke mmoja Alifahamika kwa jina la Milembe Jengamalulu anayekadiriwa kuwa na umri
wa miaka 50-55, mkazi wa Ulowa no 4 wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
umri wa miaka 50-55, amefariki dunia baada ya kuchinjwa na watu ambao
mpaka sasa hawajajulikani.
MWILI wa Marehemu Milembe Jengamalulu ukiwa
eneo la tukioKwa mujibu wa majirani tukio hilo limetokea katika mkesha
wa mwaka mpya majira ya saa moja usiku, nyumbani kwake maeneo ya Ulowa
no 4 ambapo kikongwe huyo alikuwa anaishi na mtoto wake wa kiume.
Wameeleza kuwa Wakati tukio hilo likitokea,
mtoto wake wa kiume ambaye hakutajwa jina lake (miaka 34-40) alikuwa
ameenda kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya akiwa na mkewe maeneo ya
Ulowa no 5, na wote walirudi nyumbani majira ya saa 10 na usiku ndipo
walikuta mwili wa marehemu Milembe Jengamalulu.
Baada ya kuukuta mwili huo ukiwa nje ya
nyumba huku ukiwa umetapakaa damu nyingi, huku ukionesha kuwa amechijwa
kwa kutumia panga na shoka, walitoa taarifa kwa majirani ambao
walisaidia kutoa taarifa kwa uongozi.
No comments:
Post a Comment