Wafanyabiashara
wa Soko Kuu Mjini Njombe Wamerejea Tena Kauli Yao ya Kuutaka Uongozi wa
Halmashauri ya Mji wa Njombe Kukamilisha Ukarabati wa Miundombinu ya
Maji na Umeme Ndani ya Soko Hilo.
Akiongea na tovuti hii Sokoni Hapo Baadhi ya Wafanatbiashara Hao
Wamesema Kuwa Kwa Muda Mrefu Wamekuwa Wakikabiliwa na Changamoto ya
Ukosefu wa Huduma ya Umeme na Maji Hali Inayosababisha Soko Hilo Kuwa
Chafu.
Wakielezea Suala la Usafi Ndani ya Soko Hilo Wamesema Kuwa Licha ya
Kutoa Fedha Kwa Ajili ya Kuzoa Taka Lakini Bado Zoezi la Kuzoa Taka
Hizo Limekuwa Likichelewa na Kusababisha Mlundikano wa Taka na Harufu
Mbaya Inayohatarisha Afya za Wafanyabiashara na Wateja Wanaofika Sokoni
Hapo Kwa Ajili ya Kujipatia Mahitaji Yao.
No comments:
Post a Comment