NA DIANA BISANGAO WA IRINGA
WATU
watano wanashikiliwa na polisi mkoani Iringa kwa makosa mawili tofauti
likiwemo la wakazi watatu wa dare s salaam kukutwa na pembe tano za
ndovu maeneo ya kijiji cha ngenza kata ya ikweha tarafa ya sadani wilaya
ya mufindi..
Akizungumza
na mtandao huu wa www.matukiodaima.com kamanda wa polisi mkoa wa Iringa
RAMADHANI MUNGI alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea
januari 11.
Hata
ivyo aliwataja watu hao ni RAJABU MARI (35), KADILI MOHAMED (27) na
SALOME ALOYCE(50) ambao walikuwa wakitumia gari aina ya premio lenye
namba za usajili T580 mali ya FROLIAN ELIUS mkazi wa Dar es S alaam
walikutwa na pembe hizo zenye uzito wa kilogramu 37 ambazo thamani yake
bado haijafahamika.
Wakati
huohuo jeshi la polisi Iringa linawashikilia watu wawili majina RIZIKI
KAFULILO (24) na MIRAJI NZOWA (28) wote wakazi wa mashine tatu manispaa
ya Iringa kwa kosa la kukutwa na kete 16 za madawa.
MUNGI
alisema tukio hilo lilitokea mnano tarehe 12 januari mwaka huu maeneo
ya kirabu cha pombe za kienyeji ubena kata ya mivinjeni ambapo kete hizo
zinazaniwa kuwa ni madawa ya kulevya.
Aidha
kamanda MUNGI alithibitisha kutokea kwa tukio jingine la mkazi wa
luhunga tarafa ya ifwagi wilaya ya mufindi Jina JUSTINE LUWUNGO (22)
ambaye ni mkulima kuuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa
sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kuiba kuku.
CHANZO; http://mwanaharakatimzalendo.blogspot.com/2014/01/watu-watano-matatani-iringa-wakiwemo.html#.UtfGlNIW02o
No comments:
Post a Comment