Kiwanda cha mpunga
Mmoja wa wakurugenzi, Mkurugenzi mtendaji Bwana Justin Vermaak akisoma taarifa fupi kwa waziri
Profesa
Tibaijuka akipata maelekezo ya shamba kutoka kwa mmoja wa wakurugenzi,
Mkurugenzi mtendaji Bwana Justin Vermaak ambaye alimweleza kuwa suala
la kuachia ardhi atakutana na wabia wenzake watano ili kutoa majibu muda
mfupi ujao.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka akiongea na wananchi wa Mbarali
Waziri akivuka mto Chimara
Katika
ziara hiyo waziri alijionea jinsi tani zaidi ya 1800 za mpunga
uliovunwa na mwekezaji ukiwa umehifadhiwa nje ya maghala kutokana na
kukosekana na soko ndani na nje ya nchi hivyo kufanya kiwanda kuendeshwa
kwa hasara.
Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka amemtaka Mwekezaji wa
shamba la Mpunga la Kapunga[Kapunga Rice Project]kuachia hecta 1870 za
Kijiji ili kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.
Rai hiyo
ameitoa alipofanya ziara katika shamba hilo ambalo liliuzwa hecta 7370
badala ya 5500 ambazo ndizo zilizostahili na kuacha hecta 1870 ambazo ni
eneo la kijiji kabla ya kukabidhiwa shamba la NAFCO kabla ya
kubinafsisha.
Ziara hiyo
imefanywa na Waziri ili kujiridhisha baada ya kupokea mgogoro huo kwa
muda mrefu bila majibu ya kuridhisha kutoka kwa watendaji wake hivyo
kama Waziri mwenye dhamana lazima atoe majawabu yenye uhakika badala ya
kuolea majibu ofisini.
Profesa
Tibaijuka alikutana na Uongozi wa Serikali ya kijiji kabla ya kukutana
na Mwekezaji na kuhitimisha kwa kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika
katika kijiji cha Kapunga ambao pia ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Mbarali Matayo Mwangomo,Mkuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhusein
Kiffu na wataalam mbalimbali kutoka wilayani na mkoani.
Waziri
Tibaijuka aliwashukuru wananchi wa Kapunga kwa uvumilivu wao kwani licha
ya mgogoro kudumu muda mrefu hawajafanya vurugu zozote hivyo alimtaka
Mwenyekiti wa kjiji hicho Ramadhan Nyoni kudumisha amani na upendo ili
kumaliza mgogoro huo bila uvunjifu wa sheria.
Profesa
Tibaijuka alipata maelekezo ya shamba hilo kutoka kwa mmoja wa
wakurugenzi, Mkurugenzi mtendaji Bwana Justin Vermaak ambaye alimweleza
kuwa suala la kuachia ardhi atakutana na wabia wenzake watano ili kutoa
majibu muda mfupi ujao.
Hata hivyo
Bwana Vermaak alibainisha kuwa shamba hilo linakabiliwa na changamoto ya
wizi wa mbolea na mpunga kutoka kwa baadhi ya wananchi hivyo
kuzorotesha uzalishaji wa mpunga.
Aidha
Vermaak alimwambia Waziri kuwa kuharibiwa kwa miundo mbinu ya mifereji
ya maji kilometa 14 kutoka mto Ruaha kumepelekea kupungua kwa maji
katika shamba hilo hivyo kulazimika kulima chini ya kiwango.
Pia Bwana
Vermaak amemwambia Waziri kuwa wanalazimika kukodisha mashamba kutokana
na kuombwa na wananchi wa Kapunga ingawa hakuwa wazi juu ya mikataba ya
ukodishaji kuokana na mashamba hayo kukodishwa kwa shilingi 2,880,000
kwa plot na kutakiwa kulipa mwekezaji tani 24 hadi 27 za mpunga baada ya
mavuno.
Wananchi
wameonekana kushindwa kumudu gharama za uendeshaji kauli iliyoungwa
mkono na Diwani wa Kata ya Itamboleo mheshimiwa Lwitiko Mwangosi ambaye
amesema kuwa licha ya kulipia shilingi 1,680,000 mwaka jana lakini
hakupata kitu baada ya mwekezaji kuchukukua mpunga wote aliovuna.
Baada ya
kukutana na uongozi wa kijiji na mwekezaji Waziri alihutubia wananchi na
kuwaambia kuwa hivi sasa mgogoro haupo baada ya kumwomba mwekezaji
kuachia hecta 1870 na kuwataka wananchi kuwa na subira kwani suala hilo
halitachukua muda mrefu na kama atakaidi basi taarifa ataiwasilisha kwa
Rais kwani ndiye mwenye dhamana ya kufuta hati miliki ya ardhi.
Katika
mkutano huo wanachi walipata fursa ya kuuliza maswali ambapo Emmanuel
Kapalamba alimwambia wazri kuwa vijana wamekosa ardhi ya kilimo hivyo
kufanya maisha kuwa magumu kiuchumina pia kwamba hawpati huduma za umeme
na maji licha ya miundo mbinu kupita katika kijiji chao.
Kwa upande
wa wanawake walimweleza waziri kuwa kijiji hakina zahanati kutokana na
iliyokuwapo kuporwa na mwekezaji hivyo kulazimika kutembea umbali wa
kilomita 26 ili kupata huduma za afya katika hospitali ya Chimala.
Mkutano
ulifungwa kwa waziri kuchukua baadhi ya changamoto za maji,umeme na
kilimo kuzipeleka kwa mawaziri husika ili kupata ufumbuzi wa kudumu.
Katika ziara
hiyo wazir alijionea jinsi tani zaidi ya 1800 za mpunga uliovunwa na
mwekezaji ukiwa umehifadhiwa nje ya maghala kutokana na kukosekana na
soko ndani na nje ya nchi hivyo kufanya kiwanda kuendeshwa kwa hasara
ambapo baadhi ya hecta hazijalimwa na nyingine kufanya majaribio ya zao
la soya kinyume na mkastaba.
Na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment