Kumetokea mashambulio mengine ya mabomu Kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
Maafisa
wa usalama wanasema washambulizi wawili wa kujitoa muhanga walijilipua
karibu na kituo cha kitamaduni cha Iran na kuwauwa watu 3 huku
wakiwajeruhi wengi.
Kituo cha
televisheni cha Hezbollah al-Manar pamoja na duru za kiusalama ,
zimesema kuwa kilichotokea ni mashambulizi mawili ya kigaidi huku
mshambuliaji wa kwanza akilipua mabomu aliyokuwa ametega ndani ya gari.
Punde baada ya shambulizi hilo, lengine la pili likatokea.Ni shambulizi
la hivi karibuni katika msururu wa mashambulizi katika eneo ambalo ni
ngome ya kundi la dhehebu la kishia la Hezbollah.
Bomu la pili lilikuwa limetegwa juu ya pikipiki.
Milipuko hiyo imesababisha uharibifu mkubwa wa maduka na majengo katika eneo hilo.
Ubalozi
wa Iran, ulisema kuwa hapakuwa na majeraha makubwa kwa wafanyakazi wake
wa kituo chake cha kitamaduni ambacho huenda kililengwa kwa
mashambulizi.
Mabomu hayo pia yalililipukia karibu na ofisi za ubalozi wa Kuwait, lakini umesema kuwa wafanyakazi wake hawakujeruhiwa.
Mnamo mwezi Novemba, zaidi ya watu 20 waliuawa katika mashambulizi kama haya ya kujitoa mhanga dhidi ya ubalozi wa Iran.
Tangu hapo kumeshuhudiwa mashambulizi ya mara kwa mara licha ya usalama kudhibitiwa vikali
CHANZO BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment