Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha
Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe(kushoto) alipokutana
naye ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.Katibu
Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William
Kallaghe(kushoto) aakimwelezea jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na
Michezo Bw. Leonard Thadeo(kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha
pamoja baina ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(katikati) na Katibu Mkuu wa Chama
cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe(kushoto) jana
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni
na Michezo Bi. Juliana Yassoda (kushoto) akifafanua jambo wakati wa
kikao cha pamoja baina ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) na Katibu Mkuu
wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William
Kallaghe(katikati) jana jijini Dar es Salaam.Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel (kulia) akiagana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo
wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe(kushoto) mara baada ya
kumaliza mazungumza yao jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni
na Michezo Bi. Juliana Yassoda (katikati) akiteta jambo mara baada ya
kikao chao kumalizika, kulia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini
Bw. Leonard Thadeo na kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa
Tennis Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe jana jijini Dar es Salaam.
Kutoka
kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo, Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel, Katbu Mkuu wa Chama cha Mchezo Tennis Tanzania
(TTA) Bw. William Kallaghe na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo Bi. Juliana Yassoda wakiwa katika p[icha ya pamoja mara baada ya
kumaliza kikao chao jana jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija – Wizara ya Habari.
……………………………………………………………………………………………
Na Frank Shija – WHVUM
Viongozi
wa vyama vya michezo nchini wametakiwa kutmia fursa zilizopo kukutana
na viongozi wa Serikali ili kujadili kwa pamoja namna ya kuendeleza
sekta ya michezo hapa nchini.
Rai
hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokutana Katibu Mkuu
wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania (TTA) Bw. William Kallaghe
alipomtembele ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.
Profesa
Elisante alisema kuwa ni vyema viongozi wa vyama vya michezo
kushirikiana na Serikali katika kutafuta namna ya kuendeleza michezo
nchini badala ya kukaa na kulalamikia pembeni.
Aidha
amesema kuwa milango iko wazi kwa viongozi wa vyama vuya michezo kufika
katika ofisi za Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na
kuongeza kuwa atafarijika sana akiona kasi ya viongozi hao kutembelea
Wizarani hapo ikiongezeka.
“Natao
wito kwa viongozi wa vyama vya michezo nchini wajenge utamaduni wa
kushirikiana na Serikali kupitia Wizara hii ili kutafuta namna na njia
bora ya kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini badala ya kukaa pembeni
na kuiilaumu Serikali, kwakweli hii si sawasawa” Alisema Profesa
Elisante.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania (TTA)
Bw. William Kallaghe ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ushirikiano ambao wamekuwa wanautoa kwa
vyama vya michezo hapa nchini na kusema kuwa hii inaleta faraja
kuwafanya kutokuwa wapweke.
Kallaghe
aliongeza kuwa ni vyema sasa viongozi wa vyama vya michezo wakatambua
umuhimu wa kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kuleta ufanisi katika
kutekeleza majukumu yao mbalimbali.
Aliongeza
kuwa atahakikisha anahamasisha viongozi wenzake kutumia fursa za
kukutana na viongozi wa Serikali ili kukaa meza moja na kujadiliana
namna ya kuboresha sekta ya michezo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment