Mwenyekiti wa chama cha Albino mkoa wa Morogoro Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisni kwake
Lakia Mussa Kulia] mhasibu mkuu wa chama cha Albino mkoa wa Morogoro aki copy picha za Fidhira
Fadhira kushoto mama wa watoto wa watatu akihojiwa na mwenyekiti wa chama cha Albino mkoa wa Morogoro David Mganga
Akiwa
mbele ya uongozi mzima wa chama cha Albino mkoa wa Morogoro akitakiwa
kutoa maelezo kwani alikamatwa na baadae kutolewa kwenye magazeti
akifanya biashara ya kujiuza,jambon ambalo limewadhalilisha maalbino
wenzake
Na Dustan Shekidele
BAADA ya
kunaswa na kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu'OFM' kilichopo chini
ya kampuni ya Global Publishers inayochapisha magazeti
ya Uwazi,Ijumaa,Risasi Aman na ljumaawikienda Changudoa Albino Fadhira
Omari wakati wowote kuanza sasa atafunguliwa duka kubwa na chama cha
Albino Tanzania
Hatua
hiyo imekuja baada ya Uongozi wa Juu vya chama cha Albino Mkoa wa
Morogoro kusoma moja ya magazeti ya Global Publishers yalioripiti habari
za Albino huyo kunaswa kambi ya machangudao ya Khahumba mkoani hapa
usiku wa manane akiuza mwili wake kwa bei ya shilingi elfu 7 kila
kichwa..
Baada ya
kusoma gazeti hilo mwenyekiti wa chama cha Maalbino mkoa wa Morogoro Bw
David Mganga alisaka namba ya simu za Mwandishi wa habari hizi na
kumwita ofisi za chama cha maalbino mkoa wa Morogoro, ambapo pamoja na
mambo mengine alikipongeza kikosi kazi cha OFM kwa kufanya kazi nzuri ya
kufichua maovu.
"
Nakupongeza sana kwa kazi nzuri mliofanya ya kukamata Albino akijiuza
nimekuita unisaidie mambo mawili moja naomba picha zote za tukio lile na
pili naomba unisaidi kumpata yule Albino mliomnasa"alisema mwenyekiti
huyo.
Mwandishi
wa OFM alitekeleza maombi hayo ambapo siku iliyofuata uongozi mzima wa
chama cha Albinoa mkoa wa Morogoro ambao pia ulimwalika mwandishi wa
Global Publishers ulimuweka mtu kati Fadhira ambaye kwenye maelezo yake
alidai anafanya kazi hiyo baada ya kutelekezwa na mumewe aliyeza naye
watoto watatu ambao wote hawana ulemavu huo wa ngozi.
Uongozi
huo wa mkoa ulipanga kumsomesha na baadae kumtafutia kazi kwa
kushirikiana na serikari Fadhira alikata ofa hiyo akidai kwamba ana
matatizo ya macho hivyo hatoweka kusoma na aliomba gharama hizo za
masomo zitumike kumfungulia duka jambo ambalo uongozi huo ulikubali kwa
mashariti ya Fadhira kutofanya tena biashara hiyo ya kuuza mwili wake.
Baada ya
makubaliano hayo uongozi huo uliwasiliana na uongozi wa chama cha Albino
taifa kwa utekelezaji wa kumfungulia duka Fadhira
No comments:
Post a Comment