skip to main |
skip to sidebar
AY,TUNDA MAN WAELEZEA SABABU ZA KUFANYA VIDEO NJE YA NCHI
Kumekuwepo
na malalamiko ya chini chini kutoka kwa waandaaji(Directors) wa video
za muziki wa Bongo na wadau mbalimbali, kuwa wamekua wakifanya kazi na
wasanii wa Bongo fleva tangu wanapokua wachanga(underground) kipindi
ambacho hawana pesa, lakini wakipata pesa na kuwa maarufu wanakwenda
kufanya video zao nje ya nchi.Ambapo
wakifika kwa waandaaji hao wanakua kama wanasaidiana kwa kushuti video
kali bila tatizo lolote japokuwa inakuwa ya bajeti ndogo, lakini wasanii
huwa wanafanikiwa kwa kukubalika kila sehemu ambayo video zao zinafika
na kupiga shows kibao zinazo waingizia pesa za kutosha.
Sasa waandaji
hao wanasema cha kusikitisha wasanii hao wa Bongo Fleva wakishapiga
shoo nyingi na kupata pesa za kutosha wanaenda kushuti video na
waandaaji wa nje yanchi, badala ya kurudi kwao ili wafanye video za
bajeti kubwa kitu ambacho hata wao wanakiweza.
Wameongeza juwa
wasanii hao wanapoenda nje ya nchi kushuti video wanalikosesha taifa
mapato, kwani wakifika kule wanalipa pesa nyingi za kushuti video,
wanalipia hotel, wanawalipa mamodo, wananunua vyakula, wanafanya
shopping ya mavazi, na huduma zote hizo wanakatwa kodi na nchi husika.
Je wasanii wenyewe wanalizungumziaje hilo
No comments:
Post a Comment