ONESTORY
Mgaya (31) mkazi wa kijiji cha Madaba Wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma
anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake Nesta
Mgaya mwenye umri wa miezi saba kwa kumbamiza chini kwenye barabara ya
ltami.
Kamamnda
wa polisi mkoa wa Ruvuma Deusidedit Nsimenke amesema,tukio hilo
limetokea februari 9 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi eneo la kijiji
cha Lilondo wilayani humo.
Amesema,
inadaiwa siku ya tukio mtuhumiwa na mkewe Blesila Mponda (30) pamoja na
mtoto wao Nesta walifunga safari kutoka Madaba kwenda Lilondo
kumsalimia mama wa mtuhumiwa ambapo wakati wakiwa wanarudi nyumbani
kwao wakiwa njiani kutoka nyumbani kwao na mtuhumiwa wakielekea kituo
cha mabasi Blesila aligundua kuwa amesahau kadi ya kliniki ya mtoto wao
hivyo alilazimika kumwachia mtoto mtuhumiwa ili kwenda kuchukua kadi
hiyo.
Amesema,
mtuhumiwa akiwa amembeba mwanaye kuelekea kituoni ghafla alianza
kumbamiza huyo mtoto chini kwenye barabara ya lami akiwa amemshika
miguu na kumpigiza kichwa chini ambapo wakati akiendelea kufanya unyama
huo watu waliokuwa jirani walifika na kwenda kutoa msaada ambapo
mtuhumiwa alikimbilia porini na kumwacha mtoto chini.
Amefafanua
zaidi kuwa, inadaiwa wananchi walilazimika kumkibiza mtoto huyo kwenye
kituo cha afya cha Madaba na kutokana na kuumizwa vibaya kichwani
alihamishiwa hospitali ya serikali ya Rufaa Songea ambapo alilazwa wodi
ya majeruhi kwa matibabu na siku iliyofuata aliaga dunia.
Hata
hivyo Kamanda Nsimenke ameeeleza kuwa mtuhumiwa alikamatwa siku hiyohiyo
ya tukio na anatarajiwa kupelekwa kupimwa akili ili aweze kufunguliwa
mashitaka.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
Chanzo: Mtandao-net
No comments:
Post a Comment