mbunge msigwa
akizungumza na wanahabari leo
mwandishi Kenneth
John wa matukiodaima.com Dar
Kutokana na hivi karibuni gazeti la Daily Mail linalochapishwa nchini Uingereza kuripoti kuhusu biashara haramu ya pembe za ndovu,inayokadiliwa kuwa soko la shilingi trilioni 19 za Kitanzania,Waziri wa maliasili na utalii mhe Lazaro Nyalandu alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akikanusha taarifa za chapisho hilo na huku akisema kuwa zilikuwa na mlengo wa kuichafua Tanzania.
Hivyo kutokana nakukanusha kwa waziri Nyalandu juu ya taarifa hizo imepelekea waziri kivuli wa wizara hiyo ambaye pia ni msemaji mkuu wa kambi ya upinzani Mhe,Mch Peter Msigwa kuibuka na kusema kuwa waziri Nyalandu amesahau kuwa Tanzania imejichafua yenyewe kwenye taswira ya kimataifa kutokana na biashara hiyo haramu ya pembe za ndovu.Na kuongeza Nyalandu anasahau ulimwengu wa sasa ni wakiteknolojia ambao taarifa mbalimbali juu ya biashara hiyo haramu pamoja na mauaji ya tembo zimesambaa kila mahali hasa katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi
.
Kutokana na hali hiyo Mch Msigwa amesema kuwa anashangazwa na waziri kutumia nguvu nyingi katika kupangua tuhuma dhidi ya serikali hasa katika kushindwa kwake katika kuangamiza biashara hiyo haramu,Huku akisitiza takwimu za serikali zinaonyesha mwaka 2010 tembo elfu kumi waliuwawa Tanzania pekee ambapo ni sawa na wastani wa Tembo thelathini na saba kwa siku.Aidha Msigwa ameendelea kubainisha hivi sasa Tanzania ina Tembo laki moja na hamsini hadi laki moja na sabini na kwamujibu wa takwimu hizo Msigwa amesema kunauwezekano mkubwa endapo ifikapo mwaka 2017 hadi 2018 nchi inaweza kuwa haina tembo hata mmoja,Hivyo Msigwa akasema kutokana na takwimu hizo
anashaangaa kusikia waziri akidai kuwa serikali inachafuliwa wakati takwimu zinaonyesha hali halisi ya kuendelea kwa biashara hiyo.
Aidha Mch,
Msigwa ameongeza kuwa mara nyingi waziri amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisema mtandao wa ujangili unafahamika na ni mpana na unauhusisha watu wenye nguvu za pesa na huku akiwaomba wanaojihusisha kuachana na biashara hiyo mara moja.
Hivyo
Msigwa akasema anachoona hapo kwa waziri Nyalando ni kama anawabembeleza watuhumiwa huku akijua fika wanavunja sheria.
Pamoja na hayo ameendelea kusema kauli hizo za waziri Nyalandu zinaonyesha dhahiri kuwa kuna watu ambao hawaguswi na sheria na wapo juu ya sheria.
Hata hivyo Mch Misigwa amesema kuwa kauli hizo zinaendelea kuonyesha kuwa mtandao huo umekuwa ukiogopwa.
“Majibu haya waziri yanadhihirisha kuwa mtandao huu unaolalamikiwa na kuogopwa ndio unaohusisha Ikulu,wanasiasa,
watumishi wa serikali,maafisa wanyamapori,maafisa usalama,Polisi, wanajeshi pamoja na wanyabiashara wakubwa ambao wamekuwa wakijihusisha na serikali ya CCM”Alisema Mch, Msigwa.
Akiendeendelea kufafanua Mch Msigwa amesema kitendo cha kukamata kwa shehena za meno na pembe za ndovu hakumaanishi kuwa waziri anafanya kazi kwani tembo wanakuwa tayari wamekwisha uwawa
.
Halikadharika Mch, Msigwa amesema kuwa serikali makini haiwezi kumbembeleza jangili na hali hiyo inaonyesha serikali bado
haipo makini juu ya suala hilo.
Sambamba na hayo pia amebainisha baadhi ya tuhuma ambazo serikali ya Tanzania ilituhumiwa na Gazeti la Daily Mail lakini hazikutolewa ufafanuzi na Waziri Nyalandu.
Tuhuma hizo amesema ni pamoja na watu waliokaribu na mhe Rais Kikwete wanahusika katika biashara ya meno ya tembo ndio maana serikali yake imekuwa haichukui hatua stahiki katika kukabiliana na jambo hilo,na tuhumu nyingine ni ile ya ndege iliyomleta Rais wa China kuondoka na shehena ya meno ya tembo ambayo ilipakiwa na maafisa waliokuwamo kwenye ndege hiyo,
halikadharika na tuhuma ya kuwa CCM serikali yake ni wanufaikaji wakubwa wa mradi huu kutokana wanatafuta fedha kwaajili ya uchaguzi mkuu ujao na ndio maana hawachukui hatua kwa wahusika ambao wanajulikana kwa majina na wapo mitaani wakiendelea na biashara hiyo haramu.
No comments:
Post a Comment