Bw.
Godfrey Mgimwa akiwa ameshika Passport yake aliyokuwa akiwaonesha
waandishi wa habari leo katika ofisi kuu za CCM mkoa wa Iringa
alipokutana na waandishi wa habari
Chama cha
Mapinduzi (CCM) kimekanusha madai yaliyotolewa kwenye pingamizi na
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba mgombea wao (CCM)
katika Jimbo la Kalenga, Godfrey William Mgimwa, siyo Mtanzania na
kwamba hastahili kuwania nafasi hiyo ya Ubunge katika uchaguzi mdogo
unaotarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu.
Katibu wa
CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, alisema madai yaliyotolewa na
CHADEMA hayana ukweli wowote na kwamba vipo vielelezo vinavyothibitisha
kwamba Mgimwa ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa.
"CHADEMA
wameona hiyo ni sababu kuu kwao, wamekuwa wakituma meseji, wakiingia
kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kueneza uzushi kwamba mgombea wetu
alizaliwa nje ya nchi, siyo raia na mambo kadha wa kadha. Hiyo siyo
kweli kwa sababu ushahidi upo kwamba Mgimwa alizaliwa Tanzania," alisema
Mtenga.
Passport ya kusafiria ya Bw. Godfrey Mgimwa iliyooneshwa kwa waandishi wa habari leo.
Mtenga
alionyesha vielelezo vitatu kuthibitisha maelezo hayo ambavyo ni cheti
cha kuzaliwa, hati yake ya kusafiria na nakala ya barua kutoka kwa
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kalenga, iliyowataka CHADEMA wapeleke
vielelezo kuthibitisha madai hayo.
katibu huyo wa CCM mkoa wa Iringa akiwaonesha waandishi wa habari Passport halali ya Bw. Godfrey Mgimwa.
Mgimwa
mwenyewe alisema kwamba, mbali ya kuzaliwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Iringa, lakini pia amesoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi
Wilolesi katika Manispaa ya Iringa, akasoma Azania Sekondari jijini Dar
es Salaam hadi kidato cha nne wakati elimu ya kidato cha sita aliipata
St Mary's High School ya jijini Dar es Salaam.
"Baada
ya hapo nikaenda Uingereza ambapo nilisoma katika vyuo mbalimbali.
Wakati wote huo nikisoma nimekuwa nikitumia hati ya kusafiria ya
Tanzania, siyo raia wa Uingereza kama wanavyodai kwa sababu hata Katiba
ya Jamhuri ya Muungano hairuhusu," alisema Mgimwa.
Cheti cha kuzaliwa cha Bw. Godfrey Mgimwa.
barua ambayo iliyotumwa na mkurugenzi wa uchaguzi kwenda kwa CHADEMA ili waoneshe vielelezo vya madai yao.
Katibu
huyo wa CCM mkoa wa Iringa Bw. Hassan Tenga akiwaonesha waandishi wa
habari barua hiyo kutoka kwa mkurugenzi wa uchaguzi ambayo bado
haijajibiwa na CHADEMA.
Na Riziki Mashaka, Iringa.
No comments:
Post a Comment