Mwanamke
mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Rashushi Amani Shembusho, mkazi wa
Pasua, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ametapeliwa kiasi cha
shilingi milioni 5.4 na watu wasiojulikana asubuhi ya leo, Februari 20.
Bi.
Shembusho akilia kwa uchungu baada ya kudangasnywa na watu wawili, wa
kike na wakiume ambao majina yao bado hayajafahamika. watu hao
walimpeleka katika Hoteli maarufu mjini moshi, Fresh Coach na kumtapeli
shilingi milioni 5.4 ambazo alikuwa ametoka kutoa Benki ya Uchumi ya
mjini Moshi.
Askari wa
Hoteli hiyo inayodaiwa kutumika kumtapeli mwanamke huyo akimtuliza Mama
huyo ambaye alionekana kuchanganyikiwa na tukio hilo.
Mama akilia kwa uchungu.
Msamaria
Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka Mwanamke
huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi.
Mama akisimulia tukio zima kwa wananchi waliofika katika eneo la tukio baada ya kumsikia akipinga ukunga kuomba msaada.
Msamaria
Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka Mwanamke
huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi.
Bi.
Shembusho akipanda gari la Msamaria Mwema aliyejitolea kumpeleka Polisi
kutoa taarifa hizo. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
No comments:
Post a Comment