![]() |
| Kamanda Justus Kamugisha. |
Baada ya kuwepo jambazi aliyeua watu
wanane na kujeruhi watatu wilayani Tarime mkoani Mara, wanaume wa wilaya
hiyo sasa wanarejea majumbani mwao saa 1:00 usiku wakihofia kuvamiwa na
jambazi huyo.
Hatua hiyo ya wanaume kuwahi kurejea majumbani mwao imefurahiwa na akina mama wa wilayani hapa.
Wakizungumza na mwandishi kwa nyakati tofauti katika Vijiji vya
Nyamwigura, Mogabiri, Kemakorere, Sirari, Nyamongo, Magoma , Nyarwana,
Kenyamanyori, Nyarero, Nyamwaga, Rebu, Tagota, Nyakunguru, Buhemba na
Tarime mjini, akina mama wamesema kwa sasa maduka yanayouza pombe kali
kama Konyagi maarufu 'viroba' yanafunga saa 12 jioni.
Bhoke Chacha alisema, "Kwa sasa tuna furaha sana waume zetu waliokuwa
wakirudi usiku wa manane sasa wanarejea nyumbani saa 1:00 usiku".
Naye Maria John alisema mbali na juhudi za kumsaka muuaji huyo sasa wanafurahia waume zao kuwahi kurudi nyumbani mapema.
Mkuu wa Wilaya Tarime, John Henjewele amewahimiza wananchi wilayani
hapo kushirikiana kwa pamoja katika kumsaka jambazi huyo kwa kuweza
kutoa taarifa kwa vyombo husika mara wanapomwona mtu ambaye watamtilia
mashaka.
Naye Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, Justus Kamugisha alidai msako
mkali unaendelea kumsaka jambazi huyo ambaye hadi sasa hajakamatwa na
kuomba ushirikiano kutoka kwa wananchi


No comments:
Post a Comment