Mahakimu
wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa ICC mjini The Hauge, wanatarajia
kuchukua uwamuzi muhimu Jumatano kuhusiana na hatima ya kesi ya Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Kikao
kimeitishwa kutokana na ombi la waendesha mashtaka kutaka muda zaidi ili
kuweza kufanya uchunguzi huku mawakili wa Rais Kenyatta kutaka kesi
itupiliwe mbali.
Bi
Bensouda anatarajiwa kuomba muda zaidi ili kupata mashahidi wepya na
ushadidi katika kesi yake dhidi ya Rais Kenyatta kwa uhalifu dhidi ya
ubinadamu kutokana na jukumu lake katika ghasia za baada ya uchaguzi
mkuu wa 2007.
Kwa
upande wao mawakili wa Rais Kenyata wakiongozwa na Bw Stephen Kay
watawaomba majaji kufutilia mbali kesi hiyo kwa misingi kwamba waendesha
mashtaka hawana ushahidi wa kutosha kumpata na hatia mteja wao.
Mahakimu watasikiliza hoja kutoka pande zote na kuchukua uwamuzi wao.
Akihudhuria
mkutano wea viongozi wa Umoja wa afrika mjini Addis Abba wiki iliyopita
rais Kenyatta aliupongeza umoja huo kwa kuiunga mkono serikali ya kenya
katika kesi zake mbele ya ICC, na kupelekea jambo ambalo halijawahi
kufanyika, kutathmini kanuni na utaratibu wa Mkataba wa Rome.
CHANZO:VOA
No comments:
Post a Comment