Safari yangu
hii ni kutizama maenedeleo ya Bibi Aziza Mohamed aliyekuwa akiishi
chooni baada ya nyumba yake kuezuliwa na mvua yenye upepo mkali ghafla
milangoni nakutana na kufuri.
Hata pale
nilipomwacha siku ya kwanza kufika ,Chooni ambako bibi huyo
alihamishia makazi yake pia kulikuwa na kufuri.
Nikalazimika
kwenda kwa mtendaji wa Kitongoji cha Kijiweni Abdul Msuya kupata
msaada wa kumpata Bi Aziza na safari ya kumtafuta ikaanza.
Njiani
tunakutana na maeneo ambayo yaliathirika na maji ,yakiwemo mashamba ya
migomba ,mahindi kadharika mpunga
Mwenyekiti
Msuya alinionesha kila mahala palipo pata athari ya mvua
hiyo.
Migomba
iliharibika vibaya.
Udongo
ulizolewa na kupelekwa kwenye mashamba ya Mpunga.
Hata ndizo
zilizokuwa tayari zimebeba pia ziliharibika vibaya .
Hata Bamia
ikalazimu kina mama kukata mashina ya bamia na kugeuza kuni.
Tarajio la
kuvuna mahindi pia limeingia dosari.
Baada ya safari
ya takribani nusu saa kwa mbaali namuona Bi Aziza Msuya .
Alikuwa
akiotesha maharage shambani kwake.
Baada ya
kusalimiana ikamlazimu kumalizia kwanza kuzika mbegu kwa mashimo
aliyokuwa amechimba tayari
Tukaianza
safari ya kurejeas nyumbani kwake kwa kuifuata reli.
Safari ilikuwa
ni ndefu kiasi .
Mwendo
ukaongezeka mwenyekiti wa kitongoji Bw Msuya mbele ,Bi Aziza
nyuma.
Dakika 45
zinakamilisha safari yetu na hatimaye tunafika nyumbani kwa Bi
Aziza.
Bi Aziza
anachukua funguo na kufungua moja ya chumba katika nyumba iliyoezuliwa
na upepo
Ghafla anatoka
ndani na furushi ,baada ya kumuuliza hicho nini,kwa unyonge anasema ni
matandiko ya mtoto wake Sikujua Aloyce mwenye mtindio wa
ubongo.
Anafungua
chumba kingine .
Baadae anatoka
na fungua ameshikilia mkononi anaelekea kilipo choo.
Anafungua
kufuri la mlango wa Chooni.
Anaingia na
kisha anaanza kunifahamisha vitu mbalimbali alivyohifadhi ndani ya
choo hicho ambavyo ni pamoja na Nguo zake,zaidi kilichonisikitisha ni
uwepo wa Unga na maharage ndani ya choo hicho aliyopewa kama msaada .
Tulizungumza
mengi pembeni akiwepo mwenyekiti wa kitongoji cha Kijiweni Msuya
akisikiliza kwa makini maelezo ya Bibi zaidi akieleza kuwa alikuwa
akiishi katika choo hicho hadi siku hiyo.
Chumba/Jiko.
Najaribu kuwaza ,fikiria ni Mama yako uliyemuacha pale kijijini,Bibi yako uliyemuacha kijijini kwenu,Shangaza yako,Mzazi aliyekulea yuko kwenye maisha kama haya wakati wewe uko mjini ,unauhakika wa kula milo mitatu hadi minne,unawanunulia pombe washikaji ili ujenge heshima ndugu zako pale kwenu kijijini hali yao ni hii,FIKIRIA MARA MBILI.
Natoa pole kwa Bi Aziza kisha naweka mikono yangu nyuma kisha narudi sehemu yangu ya kazi. Naacha hali ikiwa bado haijategamaa ya bibi huyu mkulima. Inaonesha misaada inatakiwa kwake na jamaa wengine wa eneo hili.
Picha na Dixon Busagaga
No comments:
Post a Comment