Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, February 24, 2014

JESHI LA POLISI MKOA WA IRINGA LAPIGA MARUFUKU WANANCHI KUHUDHURIA KWENYE MIKUTANO YA KAMPENI NA MARUNGU,MAPANGA

index
Na Datus Boniface, Jeshi la Polisi Iringa
JESHI la Polisi mkoa wa Iringa limepiga marufuku kwa Mwananchi kuhudhuria mikutano ya kampeni wakiwa na marungu na mapanga hasa wakati huu wa kampeni za kuwania kiti cha Ubunge Jimbo la Kalenga.Aidha, limewataka kuacha mara moja wataka wamiliki wa Malori kubeba wafuasi na wapenzi wa vyama vya siasa kwa lengo la kuwapeleka katika mikutano ya kampeni.Akizungumza jana na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Peter Kakamba alisema Jeshi la Polisi halitavumilia mtu atakayevunja sheria katika kipindi hiki cha Kampeni na uchaguzi.“Uzoefu tuliopata katika chaguzi ndogo za Udiwani wa Kata za Nduli, Ibumu na Ukumbi ziligubikwa na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ikiwemo wafuasi wa vyama mbalimbali kushambuliana pamoja na kutembea na marungu na mapanga”alisemaAliongeza kwamba, katika chaguzi hizo yalitokea matukio mbalimbali yakiwemo ya kuingiliana ratiba za kampeni na viwanja na pia kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga watu bila sababu za msingi au kwa hisia kwamba ni wapinzani wa vyama vyao.


Kaimu Kamanda alisema, tayari kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Kalenga zimeshaanza tangu Februali 19 na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kimezindua kampeni zake Februali 22 kwa Kata ya Kalenga.
Alisema Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha kampeni hizo zinafanyika kwa amani na utulivu ambapo pia Polisi watasimamia vizuri ulinzi siku ya uchaguzi hadi kutangazwa kwa matokeo.
Hivyo, aliwataka viongozi  wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo pamoja na wafuasi wao kufanya kampeni za kistaarabu bila fujo.
Alifafanua kuwa, kila chama kizingatie ratiba na  muda wa vibali wa kumaliza mikutano ya kampeni.
Alitumia fursa hiyo pia kuwaomba wadau wa Ulinzi na Usalama kutoa ushirikiano kama walivyofanya katika chaguzi zilizopita, kwa lengo la kudhibiti vitendo vyenye kupelekea kuvuruga kampenzi na uchaguzi kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment