Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredrick
Werema akizungumza na wajumbe wenzake wa bunge maalum la katiba
katikaka viwanja vya bunge mjini Dodoma kushoto ni Dr. Fenella Mukangara
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
NA MAGRETH KINABO –MAELEZO
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema amewataka wajumbe wa Bunge
Maalum la Katiba kuijadili Rasimu ya Katiba Mpya kwa jinsi
wanavyotaka,lakini wasiondoe misingi mikuu ya kitaifa(tunu za taifa) na
maadili ya jamii ya kuhifadhi na kudumisha mambo ya misingi hiyo.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Jaji Werema wakati akitoa semina kwa wajumbe hao
leo mjini Dodoma kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Bunge la Katiba Sura ya
83 toleo la mwaka 2014.
“
Ifanyieni Rasimu ya Katiba Mpya mnavyotaka, lakini , yana mipaka
yake. Fanyeni mnachotaka ila msifanye jambo lolote litakaloondoa uwepo
wa Jamhuri ya Muungano ,” alisema Jaji Werema.
Jaji
Werema aliyataja mambo hayo ambayo yapo katika kifungu cha 9(2) katika
sheria hiyo ambayo ni kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano, uwepo wa
Serikali ,Bunge na Mahakama, mfumo wa kiutawala wa kijamhuri, uwepo wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, umoja wa kitaifa,amani na utulivu,
uchaguzi wa kidemokrasia wa mara kwa mara katika vipindi maalum kwa
kuzingatia haki ya watu wote wenye sifa ya kupiga kura.
Mambo
mengine ni , ukuzaji na uhifadhi wa haki za binadamu, utu,usawa mbele
ya sheria na mwenendo wa sheria, uwepo wa Jamhuri ya Muungano
isiyofungamana na dini yoyote na inayoheshimu uhuru wa kuabudu .
Alisema
Jaji Werema huku aelezea kuwa itakuwa si sahihi misingi hiyo , ambayo
tume imeongozwa nayo itofautiane na Bunge Maalum la Katiba.
Jaji
Werema alitoa ufafanuzi kuhusu kifungu cha 25(1) kufuatia baadhi ya
wajumbe kutaka ufafanuzi ambao ni Tundu Lissu kuhoji kuwa hakina
uhusiano na bunge hilo na Zitto Kabwe kutaka ufafanuzi na kudai kuwa
kumekuwepo na vikundi vya vyama vina rasimu mbadala je Bunge hilo lina
mamlaka ya kuweka pembeni maoni ya wananchi.
Aliongeza kuwa Bunge Maalum litakuwa na mamlaka ya kujadili na
kupitisha masharti ya katiba inayopendekezwa, kutunga masharti ya mpito
na masharti yaokanayokama Bunge Maalum litakavyoona inafaa.
Jaji
Werema alisema kifungu hicho(20) Mamlaka ya Bunge Maalum ya kupitisha
masharti ya Katiba inayopendekezwa baada ya Rasimu ya Katiba
kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na Kupitishwa na Bunge Maalum.
Hivyo
wajumbe hao ni wawakilishi wa wananchi watafanya kazi ya kuiboresha na
baade itarudi kwa wananchi kwa ajili ya kura ya maoni.
Kuhusu suala kuwa mitaani kuna rasimu katiba mbadala alisema suala hilo ni upotoshaji.
Aidha Jaji Werema aliwataka wajumbe hao kuwasilisha hoja kwa stahaa na kupeana uhuru wa kutoa maoni.
No comments:
Post a Comment