Picha ya pamoja
Na Mbeya yetuASKARI wa vyombo vya Ulinzi na nchini
wametakiwa kutumia fursa ya maduka yenye bidhaa zenye gharama
nafuu(Duty Free shop)zilizofunguliwa katika Magereza mbali mbali ili
kupata vifaa vya ujenzi katika kujenga makazi yaliyobora nay a kudumu.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak
Abdulwazkil, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka la
bidhaa zenye gharama nafuu (Magereza Duty Free Shop) katika Gereza la
Ruanda Mkoa wa Mbeya.
Amesema
mpango wa kufungua na kuanzisha maduka hayo ni azma ya serikali ya
kuruhusu mpango huu kwa watumishi wanaohudumia katika sekta ya ulinzi na
usalama kuwasaidia kuepukana na kadhia waliokuwa wakiipata awali.
Amesema
maafisa na watumishi wakitumia vizuri fursa ya maduka hayo katika
bidhaa za vifaa vya ujenzi itasaidia kuepuka aibu inayoweza kuwapata
maaskari wengi baada ya kustaafu kazi kutokana na kukosa nyumba bora ya
kuishi.
Ameongeza
kuwa Maafisa na Askari wanaostahili kupata huduma katika maduka hayo
wanatakiwa kuzingatia masharti, kanuni na taratibu mbali mbali zilizopo
na zitakazotolewa mara kwa mara kuhusiana na utoaji wa huduma husika ili
ziweze kuleta mabadiliko makubwa sasa(Big Result Now) kutokana na kuwa
na bei nafuu kuliko maduka mengine.
Kamishina
wa Magereza Nchini, John Minja, amesema Jeshi la magereza limejipanga
kuhakikisha linasambaza maduka kama hayo nchi nzima kwa ajili ya kutoa
huduma kwa maafisa na Askari ambapo hadi sasa Jeshi hilo limefikisha
maduka Sita.
Ameyataja
maduka hayo kuwa ni pamoja na Gereza la Ruanda lililofunguliwa jana
Mkoani Mbeya, Ukonga-Dar Es Salaam,Isanga- Dodoma,Karanga- Kilimanjaro,
Chuo KPF-Morogoro na Butimba- Mwanza.
Minja
amesema kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji wa maduka hayo, wanaostahili
kupata huduma ni watumishi wa Jeshi la magereza pamoja na familia zao
ambapo utaratibu utakaotumika kupata huduma hizo ni vitambulisho vyao
vya kazi ili kuhakikisha kanuni na utaratibu wa uendeshaji wa maduka
unazingatiwa ipasavyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Transit Military Shops(Mtoa huduma ya vyombo vya ulinzi kwa
Majeshi ya Tanzania), Alfazar Meghji ametoa shukrani kwa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa
kendelea kumpa mikataba ya kufanya kazi Tanzsania.
Amesema
Military Transit Shop itaendelea kushirikiana na uongozi wa Jeshi la
Magereza katika kusambaza huduma ya Duty Free Shop katika Magereza yote
Tanzania bara ili kuhakikisha kuwa maafisa na Askari wa Jeshi la
Magereza wanaweza kupata manufaa mazuri na bora.
Hata
hivyo akitoa shukrani kwa niaba ya Wageni waalikwa katika Sherehe za
uzinduzi wa duka hilo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya,
Jaji Samweli Chocha amepongeza jitihada za jeshi hilo katika kuhakikisha
watumishi wake wanakuwa na maisha mazuri.
Ameongeza
kuwa pamoja na vigezo na masharti yaliyowekwa katika upatikanaji wa
Huduma ni vema Jeshi hilo likaangalia upya umuhimu wa wakazi
wanalizunguka eneo hilo namna ya kufaidika na bidhaa zilizomo Dukani
kutokana na kutamanishwa na ubora wake.
NA MICHUZI BLOG
|
No comments:
Post a Comment