Watu waliokamatwa kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria
Afisa uhamiaji mkoa wa Dodoma Ally Haji Amil
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP David Misime.Habari na Sylvester Onesmo, picha na Peter Simoni wa Jeshi la Polisi Dodoma.
..............................................................................
..............................................................................
Jeshi
la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu wanne raia wa Ethiopia kwa
kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria, watu hao walikamatwa kufuatia
taarifa ya raia wema waliokuwa wakisafiri nao katika basi hilo.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Dodoma DAVID MISIME – SACP amesema wahamiaji hao
wamekamatwa tarehe 18/02/2014 majira ya 16:00hrs huko eneo la Kisasa
barabara Kuu ya Dodoma – Morogoro Manispaa ya Dodoma katika basi la
Kampuni ya SIMIYU EXPRESS lenye namba za usajili T.892 AQY SCANIA
lililokuwa likiendeshwa na ATHMAN S/O SELEMAN, 40yrs, kabila Mpare,
Islam, mkazi wa Shekilango Dar es Salaam likitokea Mwanza kuelekea Dar
es salaam.
Aidha
raia hao hawakuwa na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili wala
Kiingereza bali lugha yao ya Kihabeshi, lakini pia walikutwa na tiketi
za kusafiria zenye majina tofauti ambayo sio majina yao halali ambayo ni
EMAMU, MARWA, CHACHA na JOSEPH.
Baada
ya kukamatwa basi lilifikishwa kituo cha Polisi kati na kufanyiwa
upekuzi wa kina, kuhoji baadhi ya mashahidi ambao ni abiria waliokuwa
katika basi hilo ambapo uchunguzi wa awali ulibaini kuwa,wahamiaji hao
wanafahamika kwa majina ya:
1. MISGHANEA DETAMO,
2. MAKESO WILDEMKEL,
3. GERZAN WOLDISMATI,
4. TIMULO WOLEPO,
Kondakta
wa basi aitwaye HASHIM s/o JUMA, 29yrs, Mwarabu, Islamu, mkazi wa
Magomeni Dar es Salaam naye anashikiliwa kwa mahujiano kuhusiana na watu
hao.
Wakati
huo huo watu wawili raia wa Malawi nao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi
kwa kosa la kuishi nchini bila kibali, raia hao walitambulika kwa
majina ya DENIS S/O MANDA, miaka38, Mndali na RICHARD S/O PILI, miaka
25, Mchewa wote walikuwa wakiishi Ipagala Mkoani Dodoma. Jumla ya
watuhumiwa nane wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi
kuhusiana na tukio hilo.
Kwa
upande wake Afisa uhamiaji mkoa wa Dodoma ALLY HAJI AMIL amesema
wanaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya doria kwenye nyumba
za kulala wageni na misako katika vyombo vya kusafiria ili kupambana na
wahamiaji haramu hasa katika kipindi hiki ambacho bunge la Katiba
linaendelea mkoani hapa.
Kamanda
MISIME amewaomba wakazi wa Dodoma kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi
la polisi kwa kutoa taarifa haraka iwezekanavyo wanapogundua kuwepo kwa
tukio lolote la uvunjifu wa sheria. Pia uchunguzi zaidi kubaini
mtandandao wa mawakala wa usafirishaji wa wahamiaji haramu unaendelea.
No comments:
Post a Comment