Jaji Mary Shangali akikagua gwaride la askari Polisi siku ya sheria nchini |
JAJI wa
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Mary Shangali amelaani vikali vitendo vya
unyanyasaji vinavyofanywa na jeshi la Polisi kwa wanahabari wa mjini
Iringa.
Pamoja na laana hiyo amewataka askari Polisi wawapo katika mahakama yake wazingatie taratibu za mahakama.
Aliyasema
hayo mara baada ya kupokea taarifa ya kusikitisha inayowahusisha baadhi
ya askari Polisi bila ridhaa yake kumtoa nje ya mahakama na kumfikisha
katika kituo cha Polisi mmoja wa wanahabari wanaofanya kazi zao mjini
Iringa.
Mwanahabari
huyo Frank Leonard, alifanyiwa hayo kwa kile kilichoelezwa na akari hao
kwamba alikuwa akipiga picha wakati mahakama hiyo ikiendelea.
Ilikuwa
wakati jaji huyo akisikiliza kesi ya mauaji ya mwandishi wa Channel Ten,
Daudi Mwangosi inayomkabili aliyekuwa askari wa jeshi hilo, Pasificus
Cleophace Simoni.
Kesi hiyo
ilianza kusikilizwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, Februari 13 kwa
kile kilicholezwa na upande wa mashtaka kwamba uchunguzi wake
umakamilika.
“Wameitendea
kosa mahakama hii na wamtendea kosa mwanahabari huyo; kazi waliyofanya
siyo yao , inakiuka taratibu za mahakama,” alisema.
Alisema
kama kweli mwandishi huyo alikuwa akipiga picha na kuhatarisha mwenendo
wa shughuli za mahakama, askari hao walichopaswa kufanya nikuandika memo
kwake ili achukue hatua.
“Hawatakiwi
na hawastahili kuingilia kazi nazotakiwa kufanya mimi au viongozi
wengine wa mahakama wakati mahakama ikiendelea” alisema.
Alisema mahakama inafanya kazi na wanahabari na itaendelea kufanya nao kazi huku akiwasihi Polisi kuacha kuwabugudhi.
“Siku nyingine mkija na mkaona kuna dalili
ya kufanyiwa kama haya aliyofanyiwa mwenzenu tunaomba mtoe taarifa
kwangu au kwa msajili wa mahakama ili tuchukua hatua,” alisema.
No comments:
Post a Comment