Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP akiongea na
wafanyabiashara wamiliki wa Hotel na nyumba za kulala wageni mkoani
Dodoma..
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Dodoma
FAUSTINE MWAKALINGA akiongea na wafanyabiashara wenzake
Mwenyekiti
wa wenye mahoteli na nyumba za kulala wageni mkoa wa Dodoma CHAVUMA
TARATIBU akielekeza jambo katika kikao hicho cha wafanyabiashara Mkoani
Dodoma.
MOHAMED NTEMO (Com.Ntemo) akichangia
jambo katika kikao hicho cha wafayabiashara Mkoani Dodoma
Baadhi ya wafanyabiashara wamiliki wa Hotel na
nyumba za wageni katika mkutano huo
Baadhi ya wafanyabiashara wamiliki wa Hotel na
nyumba za wageni katika mkutano huo
****************
****************
Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME (SACP) amewataka wamiliki wa Hotel na Nyumba za kulala wageni
(Guest House) kuhakikisha kwamba wageni wanaotarajia kuingia mkoani humo
ambao ni wajumbe wa bunge la Katiba linalotarajia kuanza tarehe
18/02/2014 wanakuwa salama katika kipindi hiki.
Amesema
hayo katika ukumbi wa Dodoma Hotel alipokuwa akizungumza na
wafanyabiashara ambao ni wamiliki wa Hotel na Nyumba za kulala wageni
Mkoani humo na kusisitiza kubandika namba za viongozi wa Jeshi la Polisi
Mkoa wa Dodoma ili kuweza kutoa taarifa za kihalifu pamoja na kupata
huduma haraka ya kipolisi.
Pia
Kamanda MISIME amesema kulingana na kukua kwa sayansi na teknolojia
amewashauri wamiliki wa nyumba hizo kwa baadaye waboreshe huduma zao kwa
kufunga CCTV – Camera kwenye korido, kaunta na nje ya Hotel na nyumba
zao ili kuweza kurekodi na kutunza kumbukumbu za matukio katika maeneo
yao ya biashara.
Aidha
Kamanda MISIME amesema ni lazima wamiliki wa Hotel na Nyumba za kulala
wageni waweze kubaini changamoto zinazowakabili na kutathimini kila
mmoja kama eneo lake linausalama kwa kiasi gani ikiwa ni pamoja na
kufuata sheria zote za Hotel na nyumba za kulala wageni.
Halikadhalika Kamanda MISIME amewataka wamiliki hao kushirikiana katika
kupunguza ajali za usalama barabarani pamoja na kujenga utamaduni wa
kusema familia yangu haina uhalifu.
Kamanda MISIME amesisitiza kuwa wageni wote watakaofika katika nyumba za
kulala wageni wajazwe katika vitabu vya wageni, na kama wapo wawili
asiondoke mmoja mpaka kwa ruhusa ya mwenzake kitu kitakachoweza kubaini
uhalifu utakaoweza kujitokeza.
Vilevile
ameongeza kwa kusema wahudumu wa nyumba hizo pamoja na Hotel wanatakiwa
kuwa makini kwani katika kipindi hiki ndipo matapeli na wezi huwa
wakiongezeka kwa kasi.
No comments:
Post a Comment