Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, February 17, 2014

KMKM Yashindwa kuendelea Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Ushindi Mdogo wa Mabao 2--0

 Mwamuzi wa mchezo huo akimzuiya mchezaji wa timu ya Dedebit mwenye jezi 19, asilete vurugu baada ya mchezaji wa timu yake kufanyiwa rafu na mchezaji wa timu ya KMKM, katika mchezo huo timu ya KMKM imeshinda bao 2--0. na kutolewa katika michuano hiyo kwa kufungwa mchezo wa ugenini kwa mabao 3--0,ilihitaji ushindi wa mabao 4 kwa bilo indi isonge mbele katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan.
 Wachezaji wa timu ya KMKM na wa timu ya Dedebit ya Ethiopia wakiwania mpira katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. 
 Mshambuliaji wa timu ya Dedebit ya Ethiopia akiwa na mpira na huku mchezaji wa timu ya KMKM akijaribu kumzuia katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar, timu ya KMKM imeshinda bao 2-0.
                       Golikipa wa timu ya KMKM akiokoa moja ya hatari golini kwake.

 Mshambuliaji wa timu ya KMKM akiwa na mpira akijaribu kuwapita mabeki wa timu ya Dedebit ya Ethiopia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.




 Kocha wa timu ya Dedebit ya Ethiopia Micheale Andemeskel, akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliomalizika kwa timu yake kufungwa na KMKM bao 2--0, amezungumzia mchezo huo timu ya KMKM imeonesha mchezo wa kiwango cha juu tafauti na mchezo wa awali uliofanyika Ethiopia, timu yake imeweza kushinda bao 3--0, leo timu yake imeonesha kuzindia na kucheza kiwango cha chini. 
 Kocha wa timu ya KMKM Ali Bushi akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo na timu ya Dedebit ya Ethiopia, wakati timu yake kushinda katika mchezo huo kwa bao 2--0. Timu yake imecheza vizuri lakini wameshindwa kumalizia nafasi za ushindi na kulazimishwa kutoka katoka michuano hiyo kwa kuzindia kwa bao moja na  wapizani wao kwa ushindi walioupata mchezo wa kwanza uliofanyikanchini Ethiopia wiki iliopita. 
Na kusema amelani kitendo cha kocha Salum Bausi kuiponda timu yake wakati akizungumza katika vyombo vya habari wakati wa kipindi cha michezo na mkusema timu hiyoitafungwa bao 3-0, kama ilivyokuwa mchezo wa kwanza uliofanyika Ethiopia, amekasirishwa na kitendo hicho na kusema wao wameshinda katika mchezo huo.bao2--0. kinyume na maneno yake ya kuikashifu timu yake.n  
 Afisa wa ZFA Zanzibar Mhe, Hashim Salum (Mzee wa Mbonga) akitoka katika uwanja wa amaan akiwa haamini matokeo ya mchezo huo uliofanyika katika uwanja huo, timu ya KMKM, ilicheza mchezo mzuri na kutotumia nafasi walizozipata na kuzitumia chache ndio wakabata ushindi mdogo na kushindwa kusonga mbele katka michuano hiyo kwa kuwa nyuma ya goli  moja dhidi ya wapizani wao waliopata ushmdi wa mabao matatu katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Ethiopia.

No comments:

Post a Comment