Na Mahmoud Ahmad
Serekali imeweka nia kwenye suala
zima la uwekezaji na hili linajidhihirisha wazi kwenye maboresho ya sera
na miundo ya sheria zinazohusu uwekezaji,ongezeko la mitaji kutoka nje
ya nchi pamoja na mageuzi ya kiuchumi yanaosababisha kutengamaa kwa
mfumo wa soko kwa kiwango kikubwa.
Hayo yamesemwa na waziri wa kilimo chakula na ushirika inj. Christopher Chizza kwa niaba ya Mh. Waziri mkuu wa Jamhuri ya M
uungano wa Tanzania Mizengo
Kayanza Pinda wakati akifunga Kongamano la uwekezaji kanda ya ziwa huku
akitanabaisha kuwa serekali inaendelea na juhudi za maksudi za kuweka
taratibu mbambali kuleta mabadiliko chanya katika sekta za uchumi.
Chiza alisema kuwa katika siku za
karibuni sera ya ubia kati ya serekali na sekta binafsi na sheria
zinazoitekeleza,inataka serekali na sekta binafsi kutengeneza mahusiano
yanaopelekaa mazingira chanya katika ukuwaji wa uchumi wa nchi huku
serekali ikiendelea kutoa vivutio kwenye sera za kifedha na zisizo za
kifedha kwenye sekta ya biashara ya nje.
Pia Tanzania imewekeana
makubaliano treaties dhidi ya kodi inayojirudia double taxation na nchi
za Denmark,India,Italy Norway,Sweden,Kenya,Uganda,Zambia na Finland huku
ikiridhia mikataba mbalimbali inayohusu haki na ukuaji wa uwekezaji nje
ya nchi.
Nae Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally
RUfunga alisema kuwa alisema zipo fursa nyingi zinazopatikana kwenye
ukanda huu wa ziwa ambazo zinahitaji uwekezaji katika ukuaji wa uchumi
wa taifa hivyo majadiliano yetu haya na wawekezaji yatoa fursa hizo
kuweza kutupaiasha kiuchumi kwa wakazi wa kanda yetu na Tanzania kwa
ujumla.
Rufunga alisema kuwa Kama sehemu
ya juhudi za serekali ya kutoa nchi kutoka kwenye kipato cha chini
kwenda cha kati kuanzia mwa wa fedha 2013\14 kwa kushirikiana na sekta
binafsi na wabia wa maendeleo katika kutekeleza mpango wa matokeo
makubwa sasa hasa ndio lengo la kongamano hilo la uwekezaji wa kanda ya
ziwa.
Aidha Rufunga aliwataka watendaji
wa serekali kwenye ukanda huo kuanza kubadilika na kuendana na kasi ya
serekali katika kufanikiasha ukujai wa uchumi na kuacha urasimu usio wa
lazima.
No comments:
Post a Comment