
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kufungua rasmi
ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China
iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam Tanzania, leo Feb 5, 2014 kwa ajili
ya kuwakilisha nchi za Afrika na tayari imeanza mchakato katika
kukabiliana na magugu maji katika Ziwa Viktoria sambamba na shughuli
nyingine zinazolenga utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na
majanga yanayotokana na athari za tabia nchi. Kulia ni Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.

Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia Sola Pawa ndogo maalum kwa kuchajia simu na kusomea baada ya
kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu
Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam Tanzania, leo Feb 5,
2014 kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika. Kushoto ni Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.

Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal,akikabidhiwa Nembo ya Taasisi hiyo iliyofunguliwa jijini Dar es
Salaam, leo.

Makamu wa
Rais Dkt Bilal akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi
wa ofisi hiyo baada ya kufunguliwa rasmi, eneo la Oysterbay jijini Dar
es Salaam.

Makamu wa
Rais, Dkt. Bilal, akiagana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, baara ya uzinduzi huo. Picha na OMR

No comments:
Post a Comment