Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
JESHI
la Polisi mkoani Singida linamshikilia Naomi Daud (20) mkazi wa
kitongoji cha Mahawa kata ya Mungumaji tarafa ya Unyambwa Manispaa ya
Singida kwa tuhuma ya kumuuawa mtoto wake mara baada ya kujifungua.
Imedaiwa Naomi baada ya kujifungua,alimnywesha mtoto wake maji ya mvua lita moja na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SP.Cordula Lyimo amesema
tukio hilo la kusikitisha limetokea februari nne mwaka huu usiku wa nane
huko katika kata ya Unyambwa Manispaa ya Singida.
Amesema
siku ya tukio,Naomi akiwa chumbani kwao na mama yake mzazi,alijifungua
bila kusaidiwa na mtu na mama yake alikuwa akiangalia kitendo hicho kama
sinema.
“Mara
baada ya kumaliza kujifungua,mtuhumiwa aliweza kumnywesha kichanga
hicho maji ya mvua lita moja.Maji hayo ya mvua yalitokana na mvua
iliyokuwa ikinyesha kwa wakati huo.Kichanga hicho baada ya kulazimishwa
kunywa maji hayo,alianza kutapika na haikuchukua muda alifariki
dunia”,amesema.
Kaimu
Kamanda huyo amesema Naomi na mama yake mzazi waliweza kushinda na
maiti hiyo kwa siku nzima na siku iliyofuata saa mbili usiku waliibeba
maiti hiyo na kwenda kuitupa kichakani eneo la umbali wa kilomita tatu
kutoka wanakoishi.
“Kukamatwa
kwa binti huyo kunatokana na tukio la kuokotwa kwa mtoto mchanga akiwa
amefariki dunia februari 12 saa mbili asubuhi katika eneo la Bomani
mjini hapa.Mwili wa kichanga hicho kilitelekezwa na mwanamke
asiyefahamika”,amesema.
Hata
hivyo,amesema baada ya uchunguzi kufanyika,raia wema waliweza kutoa
taarifa zilizoweza kusaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa Naomi.
Kaimu Kamanda huyo,amesema baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
No comments:
Post a Comment