Mkuu
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro (kulia) akipokea msaada
huo kwa niaba ya wananchi kutoka kwa mkurugenzi wa shirika la SUMASESU
lililopo wilayani hapo
Mkurugenzi
wa shirika la SUMASESU Bw. Egnatio Mtawa akizungumza wakati akikabidhi
msaada wa bati 25 na misumari kwa ajili ya waathirika wa kijiji cha
Ndulamo
mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza wakati akipokea msaada huo kwa niaba ya wananchi
Janga
la kuezuliwa nyumba 11 katika kijiji cha Ndulamo wilayani Makete mkoa
wa Njombe limeonesha kugusa wadau mbalimbali, ambapo shirika lisilo la
kiserikali la SUMASESU lililopo wilayani hapo limetoa msaada wa bati 25
na kilo 5 ya misumari vyote vikiwa na thamani ya tsh. 325,000/=
Akikabidhi
msaada huo hii leo Mkurugenzi wa SUMASESU Bw. Egnatio Mtawa amesema
shirika lake limekuwa linafanya kazi kwa asilimia kubwa ndani ya wilaya
ya Makete hasa na watu wazima (wasio na maradhi) hivyo wameguswa na
janga hilo na kuona njia mojawapo ya kuwasaidia ni kutoa bati na
misumari kulingana na uwezo wa shirika hilo
Bw.
Mtawa amesema kupitia matatizo mbalimbali yanayoigusa jamii ni vyema
wanamakete wakawa na mshikamano na kuwasaidia wananchi pale wanapopata
matatizo mbalimbali kwa kuwa hawajapenda kupata madhara hayo
"Tumesikia
kwenye vyombo vya habari maafa yaliyowakumba wenzetu wa Ndulamo, kwa
kweli ni janga kubwa na hawawezi kulimaliza wenyewe ila kwa mshikamano
wetu wa pamoja ni hakika tutaweza kuwasaidia kuondkana na kero hii
iliyowakumba" alisema Mtawa
Akipokea
msaada huo mbele ya viongozi wa kijiji hicho Mkuu wa wilaya ya Makete
Mh. Josephine Matiro amemshukuru mkurugenzi huyo kupitia shirika lake
la SUMASESU kwa kutoa msaada huo na kuongeza kuwa msaada huo utakuwa
msaada mkubwa kwa waathirika hao
Amesema
anaimani wapo wananchi wenye uwezo na wenye mapenzi mema ya kusaidia
kuendelea kujitokeza kwani muda bado upo na unahitajika ili usaidie
kutatua tatizo hilo mapema
"Kwa
kweli kitendo kilichofanywa na SUMASESU kama wadau wa maendeleo
wilayani Makete, ni cha kuigwa na kimesaidia sana, naomba wanamakete,
ama wananchi wenye mapenzi mema kuendelea kutoa misaada yao ya hali na
mali, si lazima uwe msaada mkubwa, hata bati moja linatosha" amesema
Matiro
Naye
mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Liliyo Tweve ameshukuru kwa kijiji chake
kupatiwa msaada huo na kusema kuwa hivi sasa kazi ya kujenga nyumba
hizo zilizoezuliwa inaendelea vizuri na msaada huo utarahisisha ujenzi
kukamilika mapema
Amesema
Maazimio ya mkutano uliofanyika jana kijijini hapo yanaendelea vyema na
inategemewa ndani ya wiki mbili zijazo kazi hiyo iwe imekwisha
No comments:
Post a Comment