Miili ya wachimba migodi haramu watano, imepatikana karibu na mgodi ambao ulikuwa hautumiki nchini Afrika Kusini.
Miili ya wanaume wanne na mwanamke mmoja ilipatikana karibu na mgodi huo katika eneo la Roodepoort, Magharibi mwa Johannesburg.Walikamatwa baada ya kuokolewa na sasa wanakabiliwa na kosa la uchimbaji haramu wa migodi.
Afrika Kusini hupoteza mamilioni ya dola katika shughuli za uchimbaji haramu wa madini kila mwaka.
Ardhi inayozingira mji wa Johannesburg ina migodi mingi ambayo haitumiki na ambayo huvutia wachimba migodi haramu kutoka katika eneo hilo na nchi jirani za ,Lesotho, Msumbiji na Zimbabwe.
Mvuto wake hasa huwa ni kwamba zinaweza kuwa na madini ya dhahabu.
Wakati nyingi ya migodi hizo hazina faida za kifedha, bado zina mabaki ya dhahabu kiasi cha kuwavutia watu wengi wasio na ajira.
Waokozi wanasema kuwa bado huenda kuna wachimba migodi haramu zaidi ndani ya migodi hiyo.
No comments:
Post a Comment