Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, February 23, 2014

MZEE GURUMO: MAISHA YANGU kwa sasa ni KULA KULALA

 
Mzee Gurumo akiwa amepozi Amana Bar.
MWANAMUZIKI ambaye kwa sasa amestaafu kuimba kwa sasa, Muhiddin Maalim Gurumo amesema kuwa, tangu atangaze kuacha rasmi shughuli za muziki maisha yake ya sasa ni kula kulala kwani hana shughuli yoyote anayofanya.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, maisha yake ya sasa ni kusubiri giza liingie na jua liwake mkono uende kinywani kwa kuwa hana biashara yoyote anayoiendesha ya kuweza kumpatia ridhiki, mara nyingi huwa anajipumzisha kwenye baa ya Amana akiifariji nafsi yake.
“Makazi yangu makubwa mimi ni kwenye baa ya Amana hapa sinywi pombe wala sivuti bangi napoteza muda saa ya kula ikifika nakula ya kulala nalala sitaki kujichosha uzeeni, wapo wengi tu wanaonitunza kuhakikisha sipati tabu kifedha,”alisema mzee Gurumo.
(STORI:MAYASA MARIWATA /GPL


No comments:

Post a Comment