Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, February 23, 2014

NAIBU WAZIRI DKT PINDI HAZARA CHANA AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI MUNGURI, KONDOA- DODOMA


 Pichani juu Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto,  Mhe. Dkt. Pindi Hazara Chana akikagua utoaji wa mafunzo katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Munguri, Kondoa, akiwa ameambatana na Uongozi wa Wilaya ya Kondoa.   
 Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana akiwa katika ziara hii ya Kikazi alipata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Munguri, kondoa ambacho ni miongoni mwa vyuo 55 vinavyotoa mafunzo ya elimu ya wananchi, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya ufundi stadi, VET 

Wakati wa ziara hii Mhe. Naibu Waziri aliiasa jamii ya Kondoa kutumia fursa hii kuwahimiza vijana kuja kupata mafunzo na ujuzi mbalimbali utakao wawezesha kujiajiri na hatimae kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, na hata kiwango cha umaskini katika jamii. 

Alisisitiza kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuimarisha  utoaji mafunzo katika chuo hiki na vingine nchini, ili kufikia vijana wengi zaidi na  kutekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM ya mwaka 2010.


 

No comments:

Post a Comment