Jina
la Ogopa Deejays limekuwa zaidi katika miaka ya karibuni nchini
Tanzania kutokana na wasanii wengi wa Bongo kufanya video na kampuni
hiyo, ambayo ilianzishwa miaka 1990 ikiwa studio ya kurekodi audio pekee
kwa wakati huo.
Kwa
mujibu wa mtandao wa GHAFLA, Ogopa deejays imesitisha mikataba ya
baadhi ya wasanii ambao ilikuwa ikiwasimamia kwa miaka kadhaa iliyopita.
Wasanii
waliopitiwa na panga hilo ni pamoja na mwimbaji mrembo Avril ambaye
taarifa za hivi karibuni zinasema anategemea kuhamishia makazi yake
Afrika Kuisni, yaliko makazi ya mchumba wake wanaetarajia kufunga ndoa
hivi karibuni.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Marya
Wasanii wengine ambao mikataba yao imesitishwa na Ogopa ni Marya, Colonel Moustapha na Kenzo.

Colonel Moustapha
Mmiliki
wa studio ya Ogopa Lucas Bikedo, ametoa maelezo kuhusu taarifa
zilizoenea za kusitishwa kwa mikataba ya baadhi ya wasanii wake,
“Kila
mara mashirika hufanya mapitio ya ndani kutathmini utendaji dhidi ya
matarajio. Wakati wa mapitio, maamuzi magumu hutakiwa
kufanyika”.Ilisema taarifa kutoka kwa Lucas baada ya GHAFLA kutaka
kupata ufafanuzi.
“Sehemu
ya matarajio yetu imekuwa ni kutafuta na kutoa vipaji ambavyo vinaweza
kushindana nje ya Afrika Mashariki. Katika siku za nyuma mfumo huu
umeweza kufanya kazi vizuri sana. Hata hivyo, sekta ya burudani
imebadilika kwa haraka na uwekezaji uliohusika kuleta mafanikio unakuwa
kila siku.
Kama
biashara, uwekezaji ni lazima ulete faida ndani ya wakati uliokusudiwa.
Hii itaruhusu uwekezaji mpya ili uchumi ukue. Na hii inawezekana tu
katika mazingira ambapo vipaji vinavyohusika vinapotambua kuwa hata kama
kuna kushinda ama kushindwa ni lazima uendele kujitahidi kadri ya uwezo
katika kazi iliyo mbele. Hakuna mbadala wa kufanya kazi kwa bidii,
malengo na nidhamu.
Mtindo
wa biashara wa sasa wa kusaini vipaji ni hatari sana na una assumptions
nyingi mno. Sehemu ya tathmini inayoendelea inahusisha na kuangalia
mtindo huu na umuhimu wake katika hali ya sasa.”
Hata hivyo Lucas hakutoa majibu ya moja kwa moja kuhusu wasanii wanaodaiwa kupoteza nafasi zao Ogopa deejays.
Source: GHALFA



No comments:
Post a Comment