Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, February 13, 2014

Okwi Ruhusa kuichezea Yanga



SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limemuidhinishamshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi kuchezea klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa ametoa taarifa muda huu kwamba, FIFA imewaandikia barua ikiwaambia Okwi ni halali kuchezea Yanga SC.
“Suala la Okwi limekwisha, ila siwezi kuzungumza zaidi kwa sasa naingia kwenye kikao, tutatuma taarifa kwa vyombo vya habari baadaye,”alisema Mwesigwa.

 TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)

No comments:

Post a Comment