Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, February 22, 2014

Sababu za wanaume kuota matiti




Kitaalamu, tatizo hilo hujulikana kama, gynecomastia nalo ni kukua kuliko kawaida kwa tishu ya kwenye titi inayojulikana kama glandular tissueTatizo la kuota matiti kwa wanaume na watoto wa kiume limekuwa kubwa katika dunia ya leo.

Inawezekana wakati unatembea njiani ukaona wanaume au watoto wadogo wa kiume wakiwa na matiti tena makubwa  ambapo watu wengi  huchukulia kama ni kawaida. Kitaalamu, tatizo hilo hujulikana kama, gynecomastia nalo ni kukua kuliko kawaida kwa tishu ya kwenye titi inayojulikana kama glandular tissue.

Tatizo hili huonekana zaidi kwa watoto wachanga na  wanaume walio katika umri wa kubalehe, lakini pia huonekana kwa watu wazima na wazee.

Ukubwa wa tatizo

Asilimia 60-90 ya watoto wachanga wanapata tatizo hili la kukua kwa matiti kwa mpito linalojulikana kitaalamu kama, transient gynecomastia kutokana na kuwepo kwa kichocheo cha aina ya estrogen kwa wingi wakati wa ujauzito wa mama.

Kati ya asilimia 4-69 ya vijana walio katika umri wa kubalehe  imeonekana wanapata tatizo hili kutokana na  kuwepo kwa wingi kwa kimeng’enyo aina ya estradiol. Mara nyingi huonekana katika umri kati ya miaka 10-12 na hupotea taratibu ndani ya miezi 18, si kawaida yake kuonekana kwa vijana walio na umri wa zaidi ya miaka 17.

Asilimia 24-65 ya watu wazima hupatwa na tatizo hili, hii hutokana na kubadilishwa  kwa wingi kwa kichocheo aina ya testosterone kuwa estradiol na kutolewa kwa uchache kwa kichocheo hiki cha testosteron kutoka kwenye korodani ziazoanza kuzeeka..Ikumbukwe ya kwamba kichocheo hiki testosteron hutengenezwa katika korodani. Kichochezi cha testosteron ndicho kichochezi kikuu cha kiume  kinachowezesha tabia za kimwili za kiume.

Nini hutokea?

Kuongezeka ukubwa wa matiti kwa wanaume hutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo unaojulikana kitaalamu kama, estrogen-androgen balance na hivyo kusababisha estrogen kutolewa kwa wingi ama kuongezeka kwa msisimko wa matiti kwa kiwango cha zaidi ya kawaida kwa kichocheo aina ya estrogen kilicho kwenye mzunguko wa damu.

Kichocheo hiki husababisha chembechembe zinazojulikana kama ductal epithelia kuongezeka kwa wingi, kurefuka na kugawanyika, kuongezeka kwa chembechembe za mafuta na kuongezeka kwa mfumo wa damu kwenye matiti hutengenezwa kutoka kwenye vichocheo vya testosteron na androgen kwa kutumia kimeng’enyo kinachojulikana kama aromatase.

Aina za tatizo hili

-Puffy nipples –Kuongezeka ukubwa wa chuchu za matiti kutokana na kuongezeka kwa tishu aina ya glandular.

No comments:

Post a Comment