Na Kenneth Ngelesi, Mbeya
MAMLAKA
ya mapato nchini TRA imewatoa hofu wafanyabishara kutumia mashine za
EFD kwani kodi inakatwa asilimia 30 ya faida baada ya kutoa gharama zote
za uendeshaji na manunuzi.
Kauli
hiyo imetolewa mwishoni mwa juma na Afisa Mwandamizi Mkuu wa Elimu wa
mamlaka ya Mapato nchini (TRA) makao Makuu Hamis Lepenza katika hotel ya
Paridise jiji hapa katika Mkutano na waandishi kutoka vyombo mbalimbali
ambao uliyo itishwa na mamlaka hiyo kwa lengo la kuwataka wandishi
wasaidie kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa mashine hizo.
Lupenza
alisema kuwa hofu ya wafanyabiashara wengi kuto taka kutumia mashine
hizo ni kuto kuwa tayari kukatwa asilimia hiyo ni kwamba wengi hawana
elimu ya juu utumiaji wa mashine hizo.
Afisa
huyo alisema kuwa wengi wao wamekuwa na malalamiko kuwa hawaja soma
hivyo kuwa nguma kwao kuzitumia miashine hizo jambo alilodai siyo la
kweli bali ni janja ya wafanyabishara kwani wana hofia mashine hizo
zitasababisha kuonyesha mauzo kuongezeka na kodi ya kulipa kuwa kubwa.
Aliongeza
kuwa kutokana makato kuwa wazi katika ulipaji wa kodi ndiyo sabababu
wafanyabiashara kutokuwa tayari kutuma mashine hizo.
Lepenzi alisema kuwa wafanyabishara wengi wamekuwa wakilala mika kuwa hawaja soma jambo hivyo uwezo wa kutumia msahine ni mgumu.
'Ndugu
zangu huyu mfanyabishara anasema hajasoma hivyo hataweza kutumia
mashine hizo lakini mtu huyo huyo unanunua simu nzuri kubwa na yenye
mambo mengi kuliko hata hiyo mashine ya EFD' alisema Lupenza.
Aliongeza
kuwa tatizo lingine lililopelekea zoezi kuwa gumu ni ugeni wa utamaduni
wa kutumia mashine hizo katika jamii yetu na siyo kigezo cha elimu kama
kinavyo tolewa na baadhi ya wafanyabishara walio wengi.
Katika hatau nyingine Afisa elimu na huduna ya mlipa kodi kutoka
makao
Makao Makuu Sigsimund Kafuru aliwataka waandishi kusaidia kutoa elimu
kwa wananchi juu ya umuhumu wa kudai risiti pindi wanapo nunua bidhaa
kwani kutochukua risiti ni kuisosesha serikali mapato na hatimaye
inashindwa kutoa huduma stahiki kwa wananchi wake.
Aidha Aliongeza kuwa ni vema wananchi wakajenga utamaduni wakudai risiti pindi wanapoa nunua bidhaa yoyote ile.
Akijibu
swali kwa waandishi habari sababu za kuteua makampuni kumi na moja tu
kupewa jukuma na kusambaza mashine hizo kutokana na kushinda tenda baada
ya kushindanisha kwa mujibu wa sheria ya manunuzi.
Tangu
mwaka 2010 serikali kupitia kwa mamlaka ya mapato nchi iliwatka
wafanyabisha kutoa risiti kwa kumtumia mashine hizo kwa sawamu ya
kwanza ikianza na wafanyabisha lakini 200,000/ lakini mpka sasa bado
kumekuwa na mvutano mkubwa baini ya ya Serikali na wafanya bishara hao.
Hata
hivyo zoezi hilo bado lina leta mvutano mamlaka hiyo imesema kuwa ipo
katika mchakato wa kuanza kutoa hudumnu ya risiti kwa kutumia mashine
hizo kwenye magari makubwa na mabasi ya kusafirishia abiria.
No comments:
Post a Comment