Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, February 9, 2014

UJENZI WA DARAJA LA DUMILA UNAENDELEA, JANA WANAKIJIJI WAMEOKOTA MAITI ILIYOSOBWA NA MAJI

Ujenzi wa daraja la Dumila ambalo lilisombwa na mafuriko mwishoni mwa mwezi uliopita kwa sasa linaendelea kutengenezwa ambapo jana iliokotwa maiti moja ya mwanaume iliyokuwa ikisobwa na maji kutokea kijiji cha jirani. Wanakijiji waliweza kuiokoa maiti hiyo na kujaribu kuitambua lakini haikufahamika na kuipeleka hospitali ya Morogoro.


Magari yakipishana upande mmoja ambao umetengenezwa kwa dharula ili kuepusha usumbufu.


Maji ni mengi yanayovuka darajani hapo.


Hapa ni mwenzo wa kusubiriana maana hamuwezi kupishana magari mawili.


Kifusi kikiendele kuchibwa.


Gari la mdau wetu ambaye ametupasha habari akisubiria kuvuka eneo la tukio.
Picha kwa hisani ya Imani Ntila wa Kajunason Blog.

No comments:

Post a Comment