Uchafu
ukiwa nyuma ya kituo cha Biafra na ukitizama picha vizuri kuna abiria
amekaa lakini cha kusikitisha nyuma yake kuna uchafu ambao unatoa harufu
mbaya na pia kuna wafanya biashara katika eneo hili. Sehemu hii imekuwa
kero kwa abiria wanaoshuka na hata wanaopanda magari kwenye hiki kituo
cha Biafra kilchopo Kinondoni kwani kuna uchafu mwingi unaotupwa na
wakazi wa eneo hilo mpaka kituo hiki kubadilishwa na kuwa dampo.
Hii
ndio hali halisi ya kituo cha Biafra kilichopo kwenye wilaya ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam kilichogeuzwa kama sehemu ya kutupia
takataka.
Jambo
la kujiuliza ina maana hapa Biafra hakuna Dampo? Au uongozi wa eneo
hili umelala mpaka kituo hiki kuwa na hali kama hii inasikitisha sana.
No comments:
Post a Comment