vigogo wa ngazi ya juu katika Idara ya wanyamapori akieleza kuwa ni
kutokana na kutoridhishwa na utendaji wao.
Ifuatayo ni Taarifa rasmi ya tamko la Waziri Nyalndu, kama alivyolisoma leo:
Leo, TAREHE 24 Februari, 2014 Natangaza kuubadili uongozi wa Idara ya
Wanyamapori ya Wizara ya maliasili na Utalii kama ifuatavyo:
Ninamuondoa Profesa Alexander Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Nachukua hatua hii kutokana na kutokuridhishwa kwangu na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika
Nachukua hatua hii kutokana na kutokuridhishwa kwangu na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika
mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini.
Aidha, hatua hii ni utekelezaji wa
Azimio la Bunge lililotolewa tarehe 22 Disemba, 2013, lililotaka
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za
uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza.
Utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul
Sarakilya kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya
Wziara ya Maliasili na Utalii kuanzia sasa.
Aidha, ninamuondoka Profesa Jafari
Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya
Wanyamapori na kumteua Dr. Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo. Hali
kadhalika, ninamteua Bwana Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi
Uzuiaji – Ujangili na anachukua nafasi ya anayeenda kuwa Kaimu
Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Vilevile, Bibi Nebbo Mwina
anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu, na
Bwana Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji
wa Wanyamapori. Pamoja na Kitengo cha Uzuiaji – Ujangili nilichokitaja
awali, hivi ni vitengo vya Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya
Maliasili na Utafiti.
Nawaagiza kwamba Wakurugenzi na
Wakuu wote wa kila Idara, kila Shirika, na Taasisi zote ndani ya Wizara
ya Maliasili na Utalii kutengeneza viashiria muhimu vya utendaji kazi
(Key Performance Indicators) na kukabidhi kwangu ndani ya siku 30
zijazo.
Viashiria hivi ni hatua ya
kufanikisha yafuatavyo, 1) Malengo ya wizara, 2) Uwajibikaji, 3)
Uwazina 4) Ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku. Ni sharti
tutekeleze mikakati ya wizara katika mifumo inayopimika, tuweze kujipima
natuweze kupimwa, natutumikie Taifa kwa uadilifu.
Kwa mtumishi wa Wizara ya Maliasili
na Utalii ikiwemo mimi mwenyewe, Lazaro Nyalandu, atapaswa kuzingatia na
kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Mwenendo (Code of
Conduct) ambazo zitapendekezwa na kupitishwa na Baraza la Wafanyakazi wa
Wizara.
Baraza hili liwe limeitishwa na
Katibu Mkuu wa Wizara kabla ya mwisho ya mwezi ujao. Azma ya kanuni
hizi ni kuwa na misingi bora ya utumishi, uwajibikaji, utu, usawa na
haki katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.
Mungu ibariki Tanzania.
Asante.
Lazaro S. Nyalandu (MB)
Wizara ya Maliasili na Utalii
24/02/2014
No comments:
Post a Comment