Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, March 19, 2014

Askari kuzichezea Yanga na Azam leo Taifa


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjFggt3nTyDzKQH9jr7c9YE7zu08vYT0gW9vzqQzM4vbAerkYBEjlhrX8f6049mN3kzwb5LO7fvY3oVjYrkjMFVOjgZ_xZaxXzVOTbkxuy9Ej1qxs9LeLhyq3SHHqQEAimpkB9EDyoLAlBd/s1600/Yanga+Vs+Azam.JPG
le shoughuli itakuwa kama hii Taifa
REFA ambaye ni askari wa jeshi la Polisi Tanzania, Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Yanga na Azam itakayochezwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.
Hashim atasaidiwa na Anold Bugado wa Singida, Florentina Zablon wa Dodoma na Lulu Mushi wa Dar es Salaam, wakati Kamisaa atakuwa Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya na mtathimini wa waamuzi ni Alfred Rwiza wa Mwanza.
Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa saa 2 asubuhi katika magari maalumu kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Ubungo Terminal, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Samora/Ohio, OilCom Ubungo, Buguruni Shell, Dar Live- Mbagala, kituo cha daladala Mwenge na Uwanja wa Taifa.
Baada ya Saa 6:00 mchana mauzo yote yatahamia Uwanja wa Taifa ambapo milango kwa ajili ya mechi itakuwa wazi kuanzia saa 7.30 mchana.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani kiingilio ni sh. 7,000.


No comments:

Post a Comment