Samuel Eto'o akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya nne Uwanja wa Stamford Bridge
Hilo lilikuwa bao la 30 la Mwafrika huyo tishio kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya
Cahill akiifungia Chelsea na kukamilisha ushindi wa jumla wa 3-1
Wachezaji wa Chelsea wakisherehekea ushindi
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba akiingia Uwanja wa Stamford Bridge na timu yake ya Galatasaray
Drogba akikumbatiana na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kabla ya mechi
Baongo la kumpa heshima yake Drogba likiwa limetungikwa Stamford Bridge wakati wa mechi
CHELSEA
itaendelea kupeperusha bendera ya England kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya
baada ya usiku huu kuitoa Galatasaray ya Uturuki kwa jumla ya mabao 3-1
Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Baada ya
kutolewa kwa Manchester City na Arsenal katikati ya wiki iliyopita,
Chelsea imejikatia tiketi ya kuingia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa
kwa kuifunga mabao 2-0 timu hiyo ya mchezaji wao wa zamani nyota, Didier
Drogba.
Mabao ya
Chelsea yamefungwa Samuel Eto'o 'Kikongwe' dakika ya nne na Gary Cahil
dakika ya 43. Katika mchezo mwingine usiku huu, Real Madrid imeifunga
Schalke mabao 3-1 Uwanja wa Santiago Bernabeu na kuwatoa Wajerumani hao
kwa jumla ya mabao 9-2 baada ya awali kushinda 6-1 ugenini. Leo mabao ya
Real yalifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 21 na 74 na lingine
Alvaro Morata dakika ya 75, wakati la Schalke limefungwa na Tim Hoogland
dakika ya 31
No comments:
Post a Comment