Mwenyekiti
wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis
Ramadhan Abdallah (kushoto) akikabidhi Ripoti ya Bodi hiyo baada ya
kukamilika kwa Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif
Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis
Ramadhan Abdallah (katikati) akisoma baadhi ya vipengele vya Ripoti hiyo
wakati wa kumkabidhi Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Zanzibar
Rashid Seif Suleiman (Mwenye Kanzu)Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya
mji wa Zanzibar. Picha na Nafisa M. Ali-WMM
………………………………………..
Na Nafisa M. Ali –WMM 17/03/2014
Bodi
ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2 leo imekabidhi rasmi
Ripoti ya ajali hiyo baada ya kumaliza kazi hiyo kwa Waziri wa Miundo
mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje
kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akikabidhi
Ripoti hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Khamis Ramadhan Abdallah amesema
kazi hiyo waliyopewa wameweza kuimaliza kwa mujibu wa siku walizopewa na
walikuwa huru bila ya kuingiliwa na mkono wa Serikali wala Taasisi
yoyote.
Aidha
alisema Bodi ilifanya kazi katika mazingira magumu lakini walichukulia
kazi hiyo niyanyumbani na niwajibu wao kufanya kwa Maslahi ya wananchi
wa Zanzibar.
Hata
hivyo alisema hapo awali kazi hiyo walipangiwa kuifanya kwa kipindi cha
mwezi mmoja lakini kutokana na uzito wa kazi hiyo na majukumu mengine
walilazimika kuomba mwezi mmoja ambapo kazi hiyo walitakiwa kuikabidhi
kesho na badala yake wameweza kuikabidhi leo.
Aidha
mwenyekiti huyo alitoa shukran zake za dhati kwa niaba ya bodi hiyo kwa
mamlaka ya Usafiri Baharini kwa ushirikiano mzuri waliouonesha kwa bodi
hiyo kwa kipindi chote cha kazi hiyo.
Kwa
upande wake Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman
ameipongeza Bodi hiyo kwa kufanya kazi bila ya upendeleo na zaidi
walizingatia uhalisia wa kazi yao na siyo kubabaishwa na Mtu.
Aidha
alisema chombo hicho hakikuundwa kwa kutafutwa nani mbaya wala mkosa wa
ajali hiyo bali kimeundwa kwa ajili ya kuangalia mapungufu yaliyopo na
kuweza kurekebishwa ili Wazanzibari wasizidi kuumia.
Hata
hivyo alisema dalili nzuri ipo katika Ripoti hiyo na kazi iliyobaki ni
kuisoma kwa kina na kisha kukabidhi katika Mikono ya Serikali kuu kwa
mujibu wa taratibu zilizopo.
Aidha aliishukuru sana bodi hiyo kwa vile ilikuwa huru na kuweza kufanya kazi kwa kina bila kizuizi cha mtu wala Serikali.
Naye
Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Tahir A.K
Abdullah amesema Wananchi hivi sasa wanasubiri kuona Serikali imefanya
nini tokea ajali hiyo imetokea ambapo aliwatoa wasiwasi kuwa haki
itatendeka kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika.
Bodi
hiyo ya Wajumbe watano ambayo iliyoundwa chini ya Sheria ya Usafiri wa
Baharini kifungu no. 4552 na 4551 ya mwaka 2006 imeundwa kufuatia ajali
ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2 iliyotokea Miezi miwili iliyopita katika
Mkondo wa Nungwi ilipokuwa ikitokea Pemba kuja Unguja.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment