Mkuu
wa wilaya ya Makete mh. Josephine Matiro (kushoto) akimkabidhi bati Bi.
Ami Mahenge, ambaye ni mmoja kati ya waathirika wa kimbunga katika
kijiji cha Ndulamo, Makete.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Josephine Matiro akiwa na waathirika hao muda mchache kabla ya kuwakabidhi.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na waathirika wa kimbunga katika ofisi za kijiji cha Ndulamo.
Kaimu
mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Peter Mwagilo
akizungumza na waathirika wa kimbunga (hawapo pichani) wakati wa
kuwakabidhi bati kama walivyoahidiwa na serikali.
Mkuu
wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza kabla ya kukabidhi
bati kwa waathirika wa kimbunga katika kijiji cha Ndulamo.
Bati zenyewe.
Kufuatia
maafa yaliyokikumba kijiji cha Ndulamo wilayani Makete mkoa wa Njombe
ya nyumba 10 kuezuliwa na kimbunga mwishoni mwa mwezi februari mwaka
huu, halmashauri ya wilaya ya Makete kwa kushirikiana na mfuko wa jimbo,
hii leo wamekabidhi bati 180 kwa waathirika wa maafa hayo
Akizungumza
na waathirika wa tukio hilo wakati wa kukabidhi bati hizo zenye thamani
ya tsh. milioni 2.5, mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro
amesema kufuatia mkutano uliofanyika baina ya serikali na wananchi wa
kijiji hicho, waligawana majukumu ambapo serikali iliahidi kutoa bati
kwa wananchi hao, na hii leo imetekelezwa
Mh.
Matiro amesema ingawa msaada huo haukuwa asilimia 100 kwa waathirika
wote lakini wamepatiwa zaidi ya robo tatu hivyo kiasi kilichobakia ni
kidogo na kuwaomba wananchi hao kumalizia gharama zilizobaki
"Mfano
mtu alikuwa ameharibikiwa nyumba yenye bati 24, hapa serikali inampa
bati 20 na hizo nne anatakiwa azigharamie yeye mwenyewe, na hii ni
kutokana na msaada huo kuhitajika katika vijiji vingine viwili vya
makete ambavyo vilikumbwa na maafa tena ili kila mmoja apate kidogo
kidogo" amesema Matiro
Amesema
kwa hivi sasa hawana budi pia kumshukuru mbunge wa jimbo la Makete
ambaye pia ni waziri wa mazingira Dkt. Binilith Mahenge kwa jitihada
zake na uongozi wa wilaya kwa ujumla kuhakikisha wananchi hao wanapata
bati hizo na kuwaomba wananchi hao kuzitumia kwa makusudi yaliyopangwa
na si kuziuza
Awali
akimkaribisha mkuu wa wilaya, kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya
wilaya ya Makete Bw. Peter Mwagilo amesema ilifanyika tahmini ya kina na
wataalamu wa halmashauri mara baada ya maafa hayo kuwakumba wananchi
hao, na hivyo kila mwananchi atapewa bati kulingana na ukubwa wa tatizo
lake
"Kwa
mfano wapo waliopata maafa kidogo wanahitaji bati chache, wengine bati
mbili hao watapata zote mbili, lakini wale waliopata maafa makubwa
watapata bati nyingi ila kila mmoja atagharamia kiasi kidogo pale
palipopelea" alisema kaimu mkurugenzi
Naye
mmoja wa waathirika hao akizungumza na mwandishi wetu baada ya
kukabidhiwa bati zake Bi. Ami Mahenge amesema anaishukuru serikali kwa
msaada huo aliopewa na kuongeza kuwa kutokana na maafa hayo yaliyomkumba
hakujua hatima ya maisha yake, ukizingatia yeye kukosa uwezo wa kifedha
lakini msaada huo umekuwa mkombozi wa maisha yake
Bi.
Mahenge ametoa wito kwa waathirika wenzake kuhakikisha wanatumia
ipasavyo msaada huo, kwa kuwa kumekuwa na kasumba ya kutumia vibaya
misaada na baadaye wanaishia kulalamik
No comments:
Post a Comment