|
|
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano) Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimweleza jambo Afisa
Habari Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Jovina Bujulu leo Mjini Dodoma. |
|
Na Jovina Bujulu-Maelezo, Dodoma
Ubora
wa elimu ya juu umeendelea kuimarika kwa kiasi kikubwa kutokana na
kuwepo kwa Taasisi za muungano kama Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bi.
Samia Suluhu Hassan wakati wa mahojiano na Afisa Habari wa Idara ya
Habari (MAELEZO) leo Mjini Dodoma.
Waziri
Samia alisema kuwa kupitia Taasisi hizo wanafunzi wenye sifa kutpoka
Tanzania Bara na Zanzibar wanapatiwa Mikopo ili kukidhi gharama za
masomo.
“kumekuwepo na ushirikiano katika suala la elimu ya juu kwa mfano kati ya wanafunzi 600 kutoka zanzibar wanaodahiliwa
na Tume ya Vyuo vikuu Tanzania, 400 kati yao wanapatiwa mikopo na Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Tanzania Bara na 200 waliosalia wanapatiwa
mikopo na Bodi ya Mikopo ya ndani ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali ” alisema Waziri Samia.
Akifafanua
zaidi kuhusu umimarikaji wa Elimu ya Juu Waziri Samia alisema kuwa,
Mwaka 1964, Zanzibar haikuwa na Chuo chochote cha Elimu ya Juu lakini
kutokana na msisitizo uliowekwa katika kuiwezesha sekta hiyo Zanzibar
imefanikiwa kuwa na vyuo vikuu 5.
Waziri
Samia Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni State University of Zanzibar (SUZA),
Zanzibar University, Chuo cha Elimu cha Chukwani, chuo cha Afya na Chuo
cha Fedha.
Serikali
zitaendelea kuhakikisha kwamba nchi inaendelea kuwa yenye umoja, Amani ,
Utulivu na Usalama ili Muungano wetu uendelee kudumu na kuimarika kwa
faida yetu na Vizazi Vijavyo
No comments:
Post a Comment