Wananchi
wa Kijiji cha Ndiwili mkoani Iringa wakishangilia helikopta iliyombeba
mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketiya Chadema, Grace Tendega
wakati ilipokuwa ikiondoka. Chadema ilifanya kampeni za uchaguzi mdogo
kijijini hapo.
Kalenga.
Wakazi wa Kijiji cha Ndiwili, Kata ya Magulilwa jimboni Kalenga, juzi
walifunga shughuli zote katika kijiji hicho na kujitokeza kwa wingi
kushuhudia mkutano wa Chadema ambao viongozi wake walitua katika kijiji
hicho kwa kutumia helikopta.
Tukio
hilo lilitokea baada ya Chadema kuanza kutumia chopa katika mikutano
yake iliyobaki. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa, Godbles Lema
alisema wanatarajia kufanya mikutano kati ya 76 hadi 100 ndani ya wiki
moja.
baadhi ya
wakazi hao wakiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ndiwili huku
baadhi yao wakitumia usafiri wa baiskeli na wengine pikipiki.
Katika
mkutano huo, wahutubiaji wakuu walikuwa Wajumbe wa Kamati Ku Chadema
Taifa, Godbles Lema ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini na
Mchungaji Peter Msigwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini na
Mgombea Ubunge, Grace Tendega.
Chopa ya Chadema ilifika katika kijiji hicho saa sita mchana na kufanya mbwembwe kwenye anga la kijiji hicho kabla ya kutua.
Baada ya
kutua na wajumbe kupanda jukwaani, viongozi hao waliwashambulia viongozi
wa CCM kwa madai kuwa wameanza kuliingiza taifa kwenye mfumo wa
kifalme, baada ya kujiwekea utamaduni wa kurithishana madaraka.
Akizungumza katika mkutano huo Lema alisema:"Taifa linaelekea kubaya
tulipokwenda, na hii inatokana na CCM kuanza mfumo wa kurithishana
madaraka," alisema.
Lema
aliwataka wakazi wa Kalenga kuupinga mfumo huo kwa vitendo na kwa kuanza
ni vyema wakampigia kura mgombea ubunge kupitia Chadema Grace Tendega.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alimshambulia
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philp Mangula akidai ni mmoja wa viongozi
wasio wakweli kwa wananchi.
Alisema
kiongozi huyo aliwadanganya wananchi kuwa chama chake kingewaengue
viongozi wote walioingia kwenye nafasi zao kwa rushwa katika kipindi cha
miezi sita na hakuna kichofanyika.
"Kama
aliwadanya wananchi kuwa angechukua hatua za kuwatimua viongozi wa CCM
walioingia kwenye nafasi zao kwa rushwa ndani ya kipindi cha miezi sita
na hadi leo hilo halijatekelezeka,atawezaje kuasaidia ninyi wananchi wa
Kalenga?alihoji Msigwa na kuongeza;
"Ninaomba
msikubali kudanganywa na viongozi hawa alipochaguliwa na kuingia
kushika wadhifa w aKaimu mwenyekiti bara alisema anarejesha maadili
ndani ya CCM na kwamba angewavua magamba wote walioingia kwenye nafasi
zao kwa rushwa ndani ya kipindi cha miezi sita...hadi leo hawajachukua
hatua,leo wanawaambia watatekeleza ahadi walizoziahidi zipi walikuw
awapi siku zote"alisema.
Msigwa
aliwataka wakazi wa Kalenga kutafanya makasa kuchagua CCM kwakuwa
viongozi wake hawana dhamira ya kweli ya kuwaaidia wananchi kupiga hatua
za maendeleo.
Kwa
upande wake Mgombea Ubunge kupitia Chama hicho Grace Tendega aliwataka
wakazi wa Kalenga kumchagua ili aweze kuwaletea maendeleo wakazi wa
Jimbo la Kalenga.
Alisema
mara atakapochaguliwa atahakikisha anafunga vizuizivya mazao
vilivyowekwa barabarani kwa ajili ya kuzuia wananchi kwenda kuuza mazao
yao nchi ya vijiji vyao.
Chanzo, mwananchi
No comments:
Post a Comment