Nani kama mwanamke?Ni mtu wa kuhangaika na kujituma siku zote na hachoki.
Mwanamke akiwa na furaha hustawisha upendo kwa watoto na familia yote kwa ujumla.
Leo ni siku ya wanawake duniani ni miaka 100 imepita sasa tangu siku hii maalumu ianze kuazimishwa duniani kote,Kwa mara ya kwanza iliazimishwa march 8 1914(8-03-2014).Ni siku maalumu ya kuwapa heshima,kuwatia faraja na kuwapongeza wanawake woteee duniani akiwemo mama yangu kipenzi kwa upendo na malezi mazuri ya kwangu na familia yetu yote kwa ujumla.
Mwanamke anahitaji kupewa haki sawa na kipaumbele ili kuweza kuinua uchumi wa nchi na pia aweze kujimudu na kuweza kusimama imara,hivyo basi Serikali na wadau wote tunatakiwa kuwapa sapoti ya kutosha wanawake wote kwenye kila sekta kisiasa,kiuchumi na hata kielimu.Ukimwelimisha mwanamke mmoja ni sawa sawa na kuelimisha jamii kwa ujumla.
IMEANDALIWA NA DJ SEK BLOG
No comments:
Post a Comment